LOWASSA APATA WAKATI MGUMU HUKO MARA AKISAKA WADHAMINI



 


Waziri mkuu wa zamani Mh.Edward Lowasa aliyeko Kanda ya ziwa kutafuta wadhamini amepata wakati mgumu alipowasili mkoani Mara baada ya makundi ya wananchi wakiwemo vijana wanawake na watoto kumfuata kila alikokwenda, wakitaka wapewe nafasi ya kumueleza kero zao jambo lililosababisha zoezi la kumdhamini kuwa gumu licha ya kufanikiwa kwa kiasi kikubwa. 

Heka heka za wananchi kutaka kuzuia msafara wa Mheshimiwa Lowasa zilianza mapema asubuhi wakati anawasili kwenye uwanja wa ndege wa Musoma ambapo vijana walizuia msafara wake kutoka kwenye la uwanja huo wakitaka wapewe nafasi ya kuonana naye. 


Baada ya waratibu wa msafara huo kufanya kazi ya ziada ya kufanikiwa kutatua changamoto hiyo Lowasa alielekea katika wilaya ya Bunda na licha ya kusimamishwa na wananchi njiani hali ilikuwa ngumu zaidi katika ofisi ya CCM wilaya ya hiyo kutokana na watu kujitokeza kwa wingi. 


Hata hivyo pamoja na maelfu ya wananchi hao walinaounga mkono safari ya matumiani kuwa na shauku ya kumueleza Mheshimiwa Lowassa shida zao alishindwa kuwasikiliza kutokana na kubanwa na kanuni na aliwaomba kuwa watulivu na kuendelea kuiombea kheri safari ya matumaini. 


Mheshimiwa Lowassa akiwa katika mkoa wa Mara ambapo alipata idadi kubwa ya wadhaamini pia amefika nyumbani kwa hayati Baba wa taifa Mwalimu Nyerere na kuweka shada la maua kwenye kaburi na pia ametembelea wilaya ya Tarime na Musoma. 


Mh.Lowassa ambaye ameshatembelea mikoa ya Mwanza Geita,Zanzibar na Pemba anaendelea na ziara yake ya kutafuta wadhamini katika mkoa wa Simiyu. 

0 maoni:

Post a Comment