Wakati Tanzania ikitarajia kufanya uchaguzi mkuu hapo Mwezi Oktoba mwaka huu,wanasiasa mbalimbali wameanza kujitokeza katika vyama vya siasa hapa nchini kuomba ridhaa ya vyama vyao katika kupeperusha bendera za vyama hivyo katika uchaguzi huo.
Hapa wilayani Tarime mkoani Mara Mbunge wa Viti Maalum kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Bi Esther Matiko amejitosa rasmi kuomba ridhaa ya Chama hicho kupeperusha Bendera ya CHADEMA katika kugombea nafasi ubunge wa jimbo la Tarime.
Katika kuhakikisha wananchi wa wilaya hiyo wanapiga kura kwa ukamilifu katika uchaguzi mkuu hapo mwezi oktoba mwaka huu,Bi Esther Matiko ametoa rai kwa wananchi wilayani humo kujiandikisha katika daftari la wapiga kura.
Mapema kabla ya mkutano wa hadhara,Bi Esther Matiko alipata mapokezi kutika eneo la Mika na kIsha kuchukua fomu ya kuomba ridhaa ndani ya chama hicho cha hicho katika ofisi za CHADEMA.
0 maoni:
Post a Comment