MTOTO MLEMAVU WA NGOZI ANUSURIKA KUUZWA HUKO TABORA



 Jeshi la Polisi mkoani Tabora limefanikiwa kumtia mbaloni mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la Masanja Mwinamila, mkazi wa kijiji cha Konanne kata ya Ugembe wilayani Nzega mkoani Tabora, akiwa katika harakati za kutafuta soko la kumuuza mlemavu wa ngozi (Albino) mtoto wa dada yake kwa fedha nyingi.


Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari mkoani Tabora kaimu kamanda wa polisi mkoani Tabora kamishina msaidizi Juma Bwire amemtaja mtuhumiwa wa tukio hilo kwa jina la Masanja Mwinamila, ambaye aliangukia katika mikono ya polisi kutokana na taarifa za wasamaria wema, na polisi kuweka mtego.
 
Aidha kaimu kamanda wa polisi Juma Bwire amesema  fedha alizo taja kumuuza binti huyo, idadi imehifadhiwa isiwe kichocheo, huku akidai kuwa, wanaendelea kumuhoji kama kuna watu anaoshirikiana nao. 

Mama mzazi wa mtoto huyo aliyenusurika Magreth Hamis (miaka sita) ambaye pia ni mlemavu wa ngozi, amesema kuwa, katika nyumba yao anaishi na watoto wake kutokana na kufiwa na mmewe walivamiwa na watu waliokuwa wameficha nyuso zao na kuanza kuwafukuza na kisha kumkamata mtoto huyo na kutokomea naye. 

Aidha kaimu kamanda Juma Bwire ameitaka jamii kutoa ushirikiano pale wanapobaini watu wanaosababisha walemavu wa ngozi kuishi kwa wasiwasi ili kukomesha vitendo vya ukatili. 

0 maoni:

Post a Comment