Wakati zoezi la uchukuaji fomu za kugombea nafasi za ubunge na udiwani kwa ajili ya uchaguzi mkuu mwaka huu likiwa limepamba moto katika vyama mbalimbali vya siasa hapa nchini,waliokuwa madiwani wapatao 10 kutoka katika vyama vya CCM na UDP wilayani Bariadi mkoani simiyu wamevihama vyao vyao na kujiunga na chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA.
Wametangaza uamuzi wa kuvihama vyama vyao katika mkutano wa hadhara wa chama hicho ulofanyika katika kijiji cha dutwa.
Katibu mwenezi wa chama hicho wilaya ya bariadi,martini moga amesema kujiunga kwa madiwani hao kutakiongezea nguvu chama hicho hasa ukizingatia kwamba sasa hivi wanaelekea katika uchaguzi mkuu.
Katika hatua nyingine mwenyekiti wa mkoa wa chama hicho Wilson Mshuda amesema chama hicho kimechukizwa na mbinu chafu zilizofanywa na aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo Andrea Chenge la kuzuia jimbo hilo lisikatwe wakati kuna wilaya hapa nchini zina wakazi wachache majimbo yao yamekatwa na kwamba kufanya hivyo ni kuwanyima wananchi kupata huduma za msingi huku mwenyekiti wa baraza la vijana mkoa huo mark malulu akiwataka vijana wa mkoa huo kutojenga uoga katika kujitokeza kugombea nafasi mbalimbali za uongozi.
0 maoni:
Post a Comment