Ulinzi mkali wa aina yake uliimarishwa leo katika Mahakama ya Kisutu jijini Dar es salaam wakati watuhumiwa 23 wa kesi ya ugaidi ambao ni wafuasi wa Jumuiya ya uamsho na mihadhara ya Kiislamu, wakiongozwa na Kiongozi wao Sheikh Farid Hadi Ahmed walipofikishwa mahakama kwa kujibu tuhuma za ugaidi.
Ulinzi huo ulihusisha vikosi mbali mbali vya Polisi ikiwemo vikosi vya Mbwa,ambapo askari walivaa mavazi maalum huku wakiwa na silaha nzito za kivita wakiwa wametanda katika eneo lote la mahakama kuimarisha ulinzi katika eneo hilo.
Katika lango kuu la Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, magari na watu wote waliokuwa wakiingia eneo hilo walikaguliwa na vifaa maalum huku wale wasiohusika hawakutakiwa kabisa kusogea eneo hilo la mahakama.
Kesi hiyo iliyokuwa ikisikilizwa bila kuruhusiwa waandishi wa habari na watu wengine imeahirishwa hadi Julai 30 mwaka huu.
0 maoni:
Post a Comment