Mwanasiasa mkongwe n aliyekuwa mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini kupitia CCM mwaka 1995 hadi 2005 Leonard Derefa amefariki dunia leo asubuhi kutokana na ugonjwa wa shinikizo la damu muda mfupi baada ya kutoka uwani kujisaidia.
Leonard Derefa( Mwanaderefa) alizaliwa mwaka 1942 katika kijiji cha Bulima wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza na hadi umauti unamfika alikuwa anaishi katika mtaa wa Mbuyuni kata ya Ndembezi katika manispaa ya Shinyanga mkoani Shinyanga.
Mmoja wa watoto wa marehemu aliyejitambulisha kwa jina la Newe Derefa amesema baba yake alifikwa na umauti leo asubuhi saa 12.30 muda mfupi baada ya kutoka uwani kujisaidia.
Newe amesema kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa na mama yake, Thereza Derefa mara baada ya mumewe kutoka uwani aliingia chumbani na badala ya kurejea kitandani alipiga magoti pembezoni mwa kitandani na kuanza kusali huku akitoka jasho jingi mwilini kiasi cha kulowana na aliamua kumgusa na kumsemesha ili kujua kitu gani kilichokuwa kikimsumbua lakini hakujibu kitu.
"Nilimchukua na kumpeleka katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga, madaktari walimpima ili kuelewa tatizo lakini walibaini tayari ameishafariki”,amesema Newe.
Jina la Leonard Derefa siyo geni katika ulimwengu wa siasa nchini Tanzania ambapo kwa wafuatiliaji wa masuala ya siasa, hasa tangu kurejeshwa kwa mfumo wa vyama vingi, watamkumbuka mwanasiasa huyo mkongwe kutokana na lafudhi yake ya Kisukuma iliyomfanya wakati mwingine apate ugumu kutamka baadhi ya maneno.
Tangu Tanzania ipate uhuru, Jimbo la Shinyanga Mjini limeongozwa na wabunge tisa ambao ni John Rupia, Bakari Msonde, Anna Tito Kachima, Ntemi Nyanda, Haninghton Mfaume, Paul Makune, Leonard Derefa, Dk Charles Mlingwa na sasa Stephen Masele.
Taarifa zaidi kuhusu msiba huu,Tutawaletea hivi punde....endelea kutembelea BLACKLISTA Blog
0 maoni:
Post a Comment