Magari ya serikali
Katibu mkuu wa chama cha madereva wa serikali nchini CMST, CHARLES MWAIHOJO, amelaani vikali tabia ya baadhi ya viongozi wa serikali kuwanyanyasa madereva wanaoendesha magari ya serikali nchini pindi wanapodai haki zao pale wanapoona zimekiukwa katika utendaji wa majukumu yao.
MWAIHOJO ameyasema hayo kando ya mkutano wa madereva mjini Dodoma na kuongeza kuwa imekuwa ni matukio ya kawaida kwa madereva kupokonywa gari na wengine kutokuthibishwa kazini kwa muda mrefu kutokana na kuwa mstari wa mbele kudai haki zao.
Kwaupande wake Makamu Mwenyekiti wa chama hicho SAIDI KAPANDE ametaja changamoto nyingine inayowakabili maderava wa serikali ni pamoja na kuwa vibarua kwa muda mrefu na hali hiyo hutumiwa kama fimbo kwao.
0 maoni:
Post a Comment