MTANDAO wa mashirika yasiyo ya kiserikali ambayo yanayojishughulisha na masuala ya kilimo endelevu – PELUM Tanzania imeanza kutoa mafunzo kwa waandishi wa habari kuhusu sera na sheria za ardhi.
Akizungumza katika mafunzo hayo ya siku tatu yaliyofanyika mjini Morogoro mratibu wa PELUM - Tanzania DONATI SENZIA amesema wameamua kutoa mafunzo hayo kutokana na changamoto mbalimbali zinazojitokeza ikiwemo za migogoro ya ardhi inayoendelea hapa nchini.
PELUM–Tanzania imeanza kutoa mafunzo kwa waandishi wa habari kutoka mikoa mitatu ya Dodoma, Iringa na Morogoro yanayohusu masuala ya ardhi , sera na sheria ili kuwajenga uwezo katika kuripoti stori hususani habari za migogoro ya ardhi.
Mada zilizotolewa katika mafunzo haya ni sera na sheria za ardhi namba 4 na namba 5 ya mwaka 1999, haki za kumiliki ardhi na maadili ya uandishi wa habari.
0 maoni:
Post a Comment