Watu 5 wamefariki dunia papo hapo na wengine watatu wamejeruhiwa wilayani Bukombe Mkoani Geita mara baada ya magari mawili kugonganana uso kwa uso katika kijiji cha Ishororo kata Bukombe mkoani humo.
Ajali hiyo imetokea jana majira ya saa 12 jioni ikihusisha magari mawili aina ya Toyota yenye namba T-302-DDT na T-402-CQJ, huku chanzo kikidaiwa kuwa mwendokasi uliosababisha madereva hao kushindwa kuchukua tahadhari.
Mganga mkuu wa hospitali ya wilaya wa Bukombe Mkoani Geita Dk. Daniel Sulusi amethibitisha kupokea maiti 5 na majeruhi watatu ambao amesema hali zao ni mbaya.
Mashuhuda wa ajali hiyo wameiambia BLACKLISTA Blog kuwa endapo madereva hao wangekuwa wanaendesha magari hayo mwendo wa kawaida wangeweza kuepusha ajali hiyo kwani eneo hilo linapitika vizuri na halina kikwazo chochote.
0 maoni:
Post a Comment