MAMA AMUUA MWANAE KWA SUMU YA MENDE

Tukio la kusikitisha sana limetokea eneo la Mbezi kwa Musuguli eneo la Bwaloni ambapo mama kwa bahati mbaya amemnywesha mwanae wa kike wa umri wa mika 3 sumu ya mende badala ya dawa ya minyoo hivyo kusababisha kifo chake.


Hii ni kwasababu mama aliweka dawa ya minyoo pamoja na sumu akaamka saa 11 alfajiri ili awahi kumpa mtoto dawa ya minyoo.

Kwa bahati mbaya badala ya kuchukua ile ya minyoo akachukua ile ya mende na kumpa mtoto kisha mtoto akaenda kulala. 

Kulipokucha vizuri wakashangaa mtoto haamki ndipo walipoenda na kumkuta katika hali mbaya.

Wakamkimbiza katika hospitali ya Bochi iliyopo Mbezi kwa Msuguli barabarani lakini walipofika waliambiwa wamechelewa sana hivyo mtoto akafariki.

Amesafirishwa Jumamosi kwenda Moshi kwa mazishi.


Wazazi wa mtoto ni watu waliookoka wakisali katika kanisa la KKKT Mtaa wa Bwaloni. Inasikitisha sana. 

0 maoni:

Post a Comment