Hapa ni katika uwanja wa CCM Kambarage mjini Shinyanga ambako leo kumefanyika sherehe za wakulima maarufu Sherehe za Nane Nane kubwa zaidi likiwa ni mashindano ya mbio za baiskeli washiriki kutoka kanda ya ziwa Victoria chini ya udhamini wa kampuni ya bia Tanzania (TBL)kupitia bia yake ya Balimi Extra Lager.
Michezo ya mbio za baiskeli iliyofanyika leo Agosti,08,2015 ni mbio za masafa marefu kwa wanaumme kilomita 220 kutoka Shinyanga kwenda Kahama na kurudi Shinyanga,mbio kwa akina mama kilomita 130 kutoka Shinyanga hadi Isaka na kurudi Shinyanga,mbio za watu wenye ulemavu kilomita 12(kuzunguka uwanja wa kambarage mara 30),mbio za akina mama wakiendesha baiskeli wakiwa wamebeba ndoo kichwani,ngoma za asili pamoja na show mbalimbali ambapo kila mshiriki ameondoka na zawadi nono.
Pia kulikuwa na shindano la kuchoma nyama lililoshirikisha bar mbalimbali mgeni rasmi akiwa ni katibu tawala wilaya ya Shinyanga Boniface Chambi kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga.
Malunde1 blog ikiwa mkoani humo,ndugu Kadama Malunde alikuwepo eneo la tukio ,ametuletea picha 35 ANGALIA HAPA CHINI
Mbio za watu wenye Ulemavu wa viungo zikiendelea,ambapo washiriki walizunguka uwanja wa CCM Kambarage mara 12 30 sawa na kilomita 12.
Ilikuwa ni burudani uwanjani...
Washindi wa kwanza hadi wa tatu mbio za baiskeli watu wenye ulemavu wa viungo vya mwili wakiwa katika picha ya pamoja.Wa kwanza kushoto ni mshindi wa kwanza Peter Thomas kutoka Luhumbo Shinyanga,katikati ni Dotto Nkingwa kutoka Luhumbo Shinyanga na George Luchagula kutoka Buchambi wilaya ya Kishapu mkoa wa Shinyanga
Washirikiwa mbio za baiskeli kundi la akina mama wanaoendesha baiskeli wakiwa wamebeba ndoo kichwani wakijiandaa kuanza shindano hilo katika uwanja wa CCM Kambarage mjini Shinyanga leo
Mashindano yalianza kwa kasi ya ajabu,akina mama wakionesha vipaji vya kuendesha baiskeli huku wamebeba ndoo ya maji kichwani bila kuangusha wala kuanguka,ni kama muujiza lakini wenyewe waliiambia malunde1 blog kuwa ujanja ni mazoezi tu
Mshindi wa kwanza Stella Nganga akimaliza mbio hizo .....
Washindi wa kwanza hadi wa tatu mbio za baiskeli za akina mama wakiwa wamebeba ndoo za maji kichwani wakiwa katika picha ya pamoja,kushoto ni mshindi wa kwanza ni Stella Nganga kutoka Maganzo,Shinyanga,katikati ni Christina Richard kutoka Masekelo Shinyanga na Elizabeth Shuli kutoka Lubaga Shinyanga.
Mshindi wa kwanza mbio za baiskeli za akina mama wanaoendesha kuhu wameweka ndoo za maji kichwani Stella Nganga akiwa amebeba mtoto wake baada ya shindano kumalizika.
Mshindi wa kwanza mbio za baiskeli masafa marefu Shinyanga hadi Isaka-Isaka -Shinyanga Tabu Charles kutoka Mwanza akimaliza kwa mbwembwe....
Mwandishi wa habari/mtangazaji wa kipindi cha Michezo na Burudani Radio Faraja ya Shinyanga Isack Edward akifanya mahojiano na mshindi wa kwanza katika mbio za masafa marefu kwa akina mama, kilomita 130 kutoka Shinyanga hadi Isaka na kurudi Shinyanga Tabu Charles kutoka mkoa wa Mwanza.
Wachezaji wa ngoma ya Mabulo ya jeshi kutoka Shinyanga wakitoa burudani,pichani wakiwa wameruka juu wakielea angani
Wananchi wakishuhudia burudani kutoka kundi la ngoma za asili maarufu Mabulo ya Jeshi yakiongozwa na msanii Wanzigiza kutoka Samuye Shinyanga.
Wachezaji wa ngoma ya Mabulo ya jeshi wakiongozwa na msanii wa nyimbo za asili Wanzigiza (kushoto) wakitoa burudani
Band ikitoa burudani
Wachezaji wa Ngoma ya Wanunguli wakifanya yao uwanjani
Wananchi wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea uwanjani
Mtoto akiangalia kwa umakini kinachoendelea uwanjani
Mshindi wa kwanza mbio za baiskeli masafa marefu kutoka Shinyanga hadi Kahama na kurudi akiingia uwanjani kwa mbwembwe
Kushoto ni mshindi wa kwanza mbio za baiskeli masafa marefu (Shinyanga/Kahama) Masunga Duba kutoka mkoa wa Mwanza na mshindi wa pili Mhindi Ng’wagi kutoka mkoa wa Simiyu wakiwa katika picha ya pamoja.
Gari la majeruhi likiwa uwanjani,walioko kwenye gari na walioshuka ni washiriki wa mbio za baiskeli Masafa marefu walioshindwa kumaliza safari yao.
Kundi la Wakali Dancers wakitoa burudani uwanjani.
Mdau wa Malunde1 blog,Anthony Mzige akichukua matukio kwa ajili ya kumbukumbu
Msanii wa nyimbo za asili Wanzigiza akiimba wimbo unaojulikana kwa jina la Tamaa,ambao anahamasisha watanzania waachane na tama ya pesa inayosababisha kuua watu wasio na hatia wakiwemo albino.
Zoezi kutoka zawadi likawadia…wa tatu kutoka kulia ni mwenyekiti wa mbio za baiskeli kanda ya ziwa Elisha Elias akizungumza wakati wa zoezi la kutoa zawadi lililoongozwa na Mgeni rasmi ambaye ni katibu tawala wilaya ya Shinyanga Boniface Chambi kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga alitoa zawadi kwa washindi zilizoandaliwa na TBL kupitia bia yake yake ya Balimi Extra Lager.
Aliyeshikilia kipaza sauti ni meneja mauzo na usambazaji kampuniya bia Tanzania(TBL) Godwin Zacharia akizungumza wakati wa zoezi la kutoa zawadi wa washindi ambapo alisema TBL imeendelea kuwa karibu na wakulima kwa kutoa bia za bei ya chini ya bia zao.
Meneja mauzo na usambazaji kampuniya bia Tanzania(TBL) Godwin Zacharia aliwahamasishaji wakulima kuendelea kununua bia za TBL kwani bei zake ni za chini
Aliyeshikilia kipaza sauti ni Mgeni rasmi ambaye ni katibu tawala wilaya ya Shinyanga Boniface Chambi kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga ambaye aliipongeza TBL kwa kuendelea kudhamini mashindano ya mbio za baiskeli kanda ya ziwa
Aliyeshikilia kipaza sauti ni meneja wa TBL mkoa wa Shinyanga Robert Kazinza akizungumza wakati wa kukabidhi zawadi wa washiriki wa mashindano hayo ya mbio za baiskeli yaliyoandaliwa na TBL
Mshindi wa pili mbio za baiskeli watu wenye ulemavu wa viungo vya mwili Dotto Nkingwa kutoka Luhumbo Shinyanga akipokea zawadi ya shilingi laki moja.
Mshindi wa kwanza alikuwa Peter Thomas kutoka Shinyanga(pichani) aliyejinyakulia kitita cha shilingi laki 1 na elfu 50,wa tatu George Ruchagula aliyeondoka na shilingi elfu 80,wan ne Richard Paulo shilingi elfu 60,wa tano Gogadi Shija elfu 50 na wengine 6-10 shilingi elfu 30.
Mshindi wa kwanza mbio za baiskeli za akina mama wakiwa wamebeba ndoo ya maji kichwani Stella Nganga kutoka Maganzo,Shinyanga akiwa amebeba mtoto wake, akipokea zawadi ya shilingi laki moja na elfu hamsini.Mshindi wa pili alikuwa Christina Giti aliyeondoka na kitita cha shilingi laki 1,mshindi wa tatu Elizabeth Shuli akiondoka na shilingi elfu 80,wan ne Jeni Shabani,elfu 60,wa tano Anastazia Kija,elfu 50,wengine 6-10 kuondoka na shilingi elfu 30.
Mshindi wa kwanza mbio za baiskeli Masafa marefu kundi la wanawake,Tabu Charles kutoka Mwanza akiwa ameshikilia kitita cha shilingi laki 7,huku mshindi wa pili Nyanzobe Masanja kutoka Shinyanga akipata zawadi ya shilingi laki 5,mshindi wa tatu Elizabeth Clement akiondoka na kitita cha shilingi laki 3,wa ,wane Tatu Maduhu kutoka Mwanza,akipata laki 2,wa 5 Rachel Simon kutoka Mwanza akipata laki moja na elfu 50,mshindi wa 6-10 kupata laki 1,na 11 hadi 17 kuondoka na kifuta jasho cha shilingi elfu 50 kila mmoja.
Mshindi wa kwanza mbio za baiskeli masafa marefu (Shinyanga/Kahama) kwa wanaume,Masunga Duba kutoka mkoa wa Mwanza akiwa ameshikilia kitita cha shilingi milioni moja.Mshindi wa pili alikuwa Mhindi Ng'wagi kutoka Simiyu aliyeondoka na zawadi ya shilingi laki 8,wa tatu Nelson Luhaga kutoka Shinyanga,laki 6,wa nne Seni Konda,shilingi laki 5,wa tano Charles Clement,shilingi laki 3,mshindi wa 6-10 kila mmoja shilingi laki 1,na 11- 20 kila mmoja aliondoka na kifuta jasho cha shilingi elfu 50.
Ukawadia muda wa zawadi kwa wachoma bora katika shindano la Balimi Nyama Choma,pichani ni bi Georgia kutoka Unique Pub ambao ni washindi wa pili,akipokea zawadi ya shilingi laki 2
Washindi wa kwanza shindano la Balimi Nyama Choma,ambao ni kutoka Lubaga Inn wakipokea zawadi ya shilingi laki tatu,mshindi wa tatu ni Free Park A waliopata shilingi laki 1,wa nne Shelaton Bar walioondoka na zawadi ya shilingi elfu 50
Washindi wa kwanza shindano la Balimi Nyama choma,wakiwa katika picha ya pamoja
Picha zote na Kadama Malunde- Malunde1 blog Shinyanga
0 maoni:
Post a Comment