Yohana Blacklista

...Usikose kukutana nami Yohana Emmanuel katika kipindi cha SAUTI YA VIJANA kupitia Radio Free Africa kilasiku ya Jumamosi inapotimu SAA 12:30 takribani dakika 30 tunakuwa tunachambua na kumulikia Yale yote mambo yanayowakumba Vijana....

Wiki hii tutakuwa na mada kubwa inayogusa kila kijana isemayo "Wahitimu wengi Hawaajiriki"...ambapo tutakuwa na vijana kutoka chuo mafunzo ya ufundi VETA Shinyanga wao watakuwa wanajadili kwa kina kuliangazia ni nini tatizo kwamba ni serikali haitoi fursa kwa vijana kuweza kupata ajira na sekta binafsi?!!,...au tatizo ni Vijana wao wenyewe binafsi hawajishughulishi kuweza kupata ajira!!??,..

Yote haya utayasikia na kuweza kupata kusikiliza Hadithi fupi ya kijana mjasiriamali ambapo wiki hii tutakuwa na Kaka Yona E Yona kutoka Ipuli,Tabora atakuja kutujulisha ni vipi kwanini mafanikio changamoto na shauri lake kwa vijana wenzake wasio na ajira.

Pia Tutamsikia Kaka Simon Appolinary kutoka Tinde,mkoani Shinyanga na Ndugu Wendelini Mkolwe kutoka Njombe wao watakuwa na machache yakuweza kuzungumza kwa Vijana wakitanzania....kumbuka Nchi ni yetu,Tanzania ni yetu na Nguvu ni zetu Tunaweza Tukithubutu,.....Usikose!!!

0 maoni:

Post a Comment