HAYA NDIYO MAJIMBO YALIYOBAKI NA WAGOMBEA WAKE!!!


Kamati kuu ya Chama Cha Mapinduzi kimeteua wagombea tisa wa nafasi ya ubunge katika majimbo ya uchaguzi tisa kati ya 11 yaliyorudia uchaguzi Agosti 13 mwaka huu huku mawaziri wengine watatu wakimwagwa.

Hatua hiyo ya CCM imefikiwa baada ya kamati kuu ambayo inaongozwa na mwenyekiti wa chama hicho rais Jakaya Kikwete kupitia na kujadili majina ya wagombea waliopita katika nafasi hiyo ambapo mawaziri walioshindwa kupenya kwenye kura za maoni na hata uteuzi wa kamati hiyo ni waziri wa mifugo na uvuvi, Dk. Titus Kamani, Busega waziri wa afya na ustawi wa jamii Dk. Seif Rashid na waziri wa mazingira, Biligith Mahenge Makete.

Nape amesema majimbo mawili ya mkoani Singida na Manyara bado yanajadiliwa na kuhusu malalamiko ya wagombea, amesema yote yamefanyiwa kazi kwa kufuata kanuni na taratibu za ngazi zote za chama na kwamba kura za maoni siyo kigezo pekee kuwania nafasi ya ubunge hivyo kuna taratibu kanuni za vikao mbalimbali vya chama, tathimini imefanywa na kusimamisha waliokidhi.

Wakati malalamiko yakiendelea dhidi ya wagombea walioshindwa na waliokatwa na chama hicho baadhi ya vijana wa chama hicho wamewataka watanzania na wanachama wa CCM kuendelea kuwa wamoja na mshikamano kwani mwezi Octoba siyo mbali.


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) taifa leo Agosti 17, 2015 katika kikao chake cha siku moja kilichofanyika katika Ofisi Ndogo za Makao Makuu ya CCM Lumumba jijini Dar es Salaa chini ya Mwenyekiti wa CCM Rais Dokta Jakaya Mrisho Kikwete imefanya uteuzi wa Wagombea Ubunge katika majimbo 11 nchini yaliyokuwa yamebakia.
Wagombea Ubunge walioteuliwa na majimbo yao kwenye mabano ni:-
1.    Ndugu Jerry Slaa                               -        (Ukonga) Dar es Salaam
2.    Ndugu Edward Mwalongo                   -        (Njombe Kusini) Njombe
3.    Ndugu Venance Mwamoto                           -        (Kilolo) Iringa
4.    Ndugu Raphael Chegeni                      -        (Busega) Simiyu
5.    Ndugu Edwin Ngonyani                      -        (Namtumbo) Ruvuma
6.    Ndugu Mohamed Mchengerwa            -        (Rufiji) Pwani
7.    Ndugu Norman Sigara                         -        (Makete) Njombe
8.    Ndugu Martin Msuha                          -        (Mbinga Vijijini) Ruvuma
9.    Ndugu Joel Makanyanga Mwaka           -        (Chilonwa) Dodoma

Imetolewa na:-


Nape Moses Nnauye,    
KATIBU WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA,
ITIKADI NA UENEZI
17/08/2015

0 maoni:

Post a Comment