ZAIDI YA ABIRIA 150 WA MV SERENGETI WAOKOLEWA KUFA MAJI,BUKOBA!!!



Zaidi ya abiria 150 waliokuwa wakisafiri na meli ya Mv Serengeti inayofanya safari zake kutoka Mwanza hadi Bukoba wamenusurika kifo mara baada ya meli hiyo kukumbana na upepo mkali na kushindwa kutia nanga katika bandari ya Bukoba.

Meli hiyo iliyokuwa ikitokea jijini Mwanza kuelekea mjini Bukoba ambapo ilikumbana na upepo mkali ndani ya ziwa Victoria na kushindwa kutia nanga katika bandari ya Bukoba na kusababisha nahodha wa meli hiyo kuirudisha majini mpaka upepo ulipo tulia ndipo ilifanikiwa kutia nanga katika bandari ya Bukoba majira ya saa tano asubuhi.

Wakizungumza mara baada ya meli hiyo kutia nanga katika bandari ya Bukoba baadhi ya wananchi wamesema meli hiyo ilianza kuyumba majini majira ya saa kumi namoja alfajiri hali ambayo imewatia wasiwasi ambapo wamekaa majini kwa zaidi ya saa sita ndipo walipofanikiwa kutoka majini huku wakiwa wana hali mbaya kisaikolojia.

Nahodha wa meli hiyo Bembele Mwita amesema kuwa meli hiyo ilikuwa haina tatizo lolote la kiufundi bali upepo mkali ulikuwepo ndani ya ziwa Victoria ndio ulichangia kwa kiasi kikubwa na kukwamisha meli hiyo na kushindwa kutioa nanga katika bandari ya Bukoba. 

Ni takribani miezi miwili imepita meli ya Mv Serengeti ianze kufanya kazi kama mbadala wa meli ya Mv Victoria baada ya kusimamishwa kwa ajili ya matengenezo.


0 maoni:

Post a Comment