VYAMA VINGINE VYA SIASA VYA MUUNGA MKONO LOWASSA

Wakati vyama vinne vya upinzani nchini Tanzania vinavyounda Muungano wa UKAWA, vimempitisha Edward Lowassa kugombea urais, vyamavingine viwili vya SAU na APPT-Maendeleo vimetangaza kumuunga mkono mgombea huyo katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25 mwaka huu. 





Katibu Mkuu wa SAU, Ali Kaniki alisema chama hicho kimefikia uamuzi wa kuunga mkono umoja huo kutokana na nafasi kubwa iliyopo ya kushika dola. Kaniki alisema kwa sasa wana wanachama zaidi ya 500,000 nchi nzima, hivyo wanaamini kuwa na mchango katika harakati hizo.Mwenyekiti wa APPT-Maendeleo, Peter Mziray alisema chama hicho kinaamini mabadiliko kupitia kambi ya upinzani, hivyo wameamua kuunga mkono UKAWA.

Katika upande mwengine, Chama cha Wananchi CUF kimeunda kamati ya muda,itakayodumu kwa miezi 6 ili kusimamia nafasi za uongozi kufuatia kujiuzulu kwa Mwenyekiti wake, Profesa Ibrahim Lipumba .Hatua hiyo ilitangazwa Jijini Dar es Salaam jana,na katibu mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad wakati wa mkutano na waandishi wa habari baada ya kumalizika kwa kikao cha dharura cha baraza kuu la uongozi kilichoitishwa kujadili hatua ya kujiuzulu Lipumba.

Maalim Seif amesema, kutokana na kanuni za CUF,wameafikiana kwa pamoja kuunda kamati hiyo itakayosimamia chama kwa kipindi cha miezi sita na baadae kufanyika uchaguzi wa nafasi hiyo ya uenyekiti. Amesema kamati hiyo itakuwa chini ya katibu mkuu huyo na mwenyekiti wake atakuwa ni mbunge wa Afrika Mashariki kutokana chama hicho Mh. Twaha Taslima

0 maoni:

Post a Comment