Mawaziri wakuu wastaafu Edward Lowassa na Fredrick Sumaye wakiwa Shinyanga hivi karibuni..
Waziri Mkuu Mstaafu wa Serikali ya awamu ya Tatu nchini Tanzania mheshimiwa Frederick Sumaye ametangaza rasmi kujiondoa kutoka Chama cha Mapinduzi CCM na kujiunga na UKAWA.
Sumaye ametangaza uamuzi huo leo katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika jijini Dar es salaam ambapo amesema anajiunga na UKAWA lakini ni chama kipi itakujulikana mbele ya safari
Sumaye anakuwa Waziri Mkuu Mstaafu wa pili kujiunga na UKAWA baada ya Waziri mkuu wa awamu ya nne Mh.Edward Lowassa kuachana na CCM na kujiunga Chadema kupitia UKAWA.
Amesema yeye kwenye CCM haondoki ili kukidhoofisha chama hicho, bali anaondoka ili kiimarike, maana yeye anajihisi ni mmoja kati ya makapi yanayotajwa na CCM
Sumaye amesema amefikia hatua hiyo baada ya kuchoshwa na uvunjaji wa kununi ndani ya CCM ikiwemo katika harakati za kumteua mgombea wa Urais kwa upande wa CCM akidai mwenyekiti wa chama hicho Jakaya Kikwete alitumia ubabe katika kuwaingiza watu wake tano bora.
Sumaye amesema atatangaza baadaye chama ambacho amejiunga nacho ndani ya UKAWA.
0 maoni:
Post a Comment