Na Kadama Malunde-Malunde1 blog Shinyanga
Kulia ni kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga SACP Justus Kamugisha akizungumza na waandishi wa habari leo asubuhi(hawapo pichani)-Picha na Kadama Malunde- Malunde1 blog
Kamanda Justus Kamugisha akizungumzana waandishi wa habari leo
Katika hali isiyokuwa ya kawaida mwanafunzi wa kidato cha pili katika shule ya sekondari Nyasubi wilayani Kahama mkoani Shinyanga Ally Jacob(15-18) ameuawa kwa kuchomwa mkasi shingoni wakati akimsaidia mwanafunzi mwenzake Roda Robson(16) asibakwe na kundi la vijana.
Akizungumza na waandishi wa habari leo kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga SACP Justus Kamugisha amesema tukio hilo limetokea jana saa tisa alasiri katika maeneo ya Nyasubi mjini Kahama.
Akifafanua kuhusu tukio hilo amesema mwanafunzi Ally Jacob mkazi wa Nyakato mjini humo akiwa njiani kuelekea nyumbani, aliuawa kwa kuchomwa kitu chenye ncha kali (mkasi) sehemu za shingoni na Mabula Sakala Makoye(18) mwanafunzi wa Shule ya sekondari Kishimba iliyoko mjini Kahama.
“Marahemu alikuwa akimsaidia mwanafunzi mwenzake Roda Robson asibakwe na Samson Lucas(19) mkazi wa Nyasubi na Masunga Nyerobi(17) mkazi wa Majengo Kanisani mjini Kahama,akachomwa mkasi na na Mabula Sakala Makoye ”,ameeleza Kamugisha.
Kamanda Kamugisha amesema vijana hao walikuwa wanataka kumbaka mwanafunzi wa kike aitwaye Roda,ndipo Ally Jacob akaamua kumsaidia mwanafunzi mwenzake na kuchomwa kitu chenye ncha kali shingoni na kufariki dunia wakati akipelekwa hospitali kwa ajili ya matibabu.
Ameongeza kuwa tayari wahusika wa tukio hilo wanashikiliwa na jeshi la polisi kwa ajili ya hatua zaidi za kisheria.
0 maoni:
Post a Comment