
Chopa iliyombeba naibu waziri wa fedha namgombea ubunge jimbo la Iramba
Magharibi,Mwigulu Nchemba na mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa
Mwanza Anthony Diallo leo jioni waliokuwa wameambatana na mbunge wa Viti
maalum mkoa wa Shinyanga mheshimiwa Azza Hilal ikitua katika eneo la
Ngokolo Mitumbani kata ya Ngokolo mjini Shinyanga kwa ajili ya mkutano
wa hadhara kumnadi mgombea urais wa CCM Dk John Pombe Magufuli,mgombea
ubunge jimbo la Shinyanga mjini mheshimiwa Stephen Masele na mgombea
udiwani wa kata hiyo Emmanuel Mlimandago Dominic-Picha zote na Kadama
Malunde- Malunde1 blog
Mheshimiwa Mwigulu Nchemba akiwapungia mkono wananchi wa Shinyanga
waliojitokeza leo Oktoba 12,2015 katika mkutano wa hadhara eneo la
Ngokolo Mitumbani mjini Shinyanga.
Akiwa Shinyanga Mwigulu Nchemba aliwaasa wakazi wa Shinyanga kutopoteza
kura zao kwa kuchagua wagombea wa upinzani bali wachague rais,wabunge na
madiniwa wa CCM huku akimwelezea mgombea ubunge wa Shinyanga mjini
Stephen Masele kuwa ni jasiri,msikivu,mchapakazi,mwenye uzoefu wa
kazi,muungwa,mwadilifu na mwenye kiu ya kuwaletea maendeleo wananchi
hivyo wampe kura na kwamba ndiye mgombea pekee aliyepata mafunzo mengi
ya uongozi.
Mheshimiwa Mwigulu Nchemba akiwahutubia wakazi wa Shinyanga leo jioni
ambapo pamoja na mambo mengine aliwataka wananchi kutunza kadi zao za
kupigia kura na kujitokeza kwa wingi kuchagua wagombea wa CCM
Kushoto ni mgombea ubunge jimbo la Solwa Mheshimiwa Ahmed Salum akiteta
jambo na mgombea ubunge jimbo la Shinyanga mjini mheshimiwa Stephen
Masele
Meza kuu wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea kwenye mkutano
Mheshimiwa Mwigulu Nchemba pia aliwataka watanzania kupiga kura kwa
kutumia vigezo mbalimbali ikiwemo uwezo wa uchapa kazi wa
wagombea,uadilifu wao ambapo alielekeza sifa hizo kwa wagombea wa CCM
akiwemo John Pombe Magufuli
Mheshimiwa Nchemba alisema kuwa mgombea urais wa Ukawa Edward Lowassa na
wenzake wamehama CCM kwa sababu ya hasira ya kukosa urais kupitia CCM
na kwamba CCM siyo mbaya...na kama ingekuwa mbaya wasingezunguka nchi
nzima kusaka wadhamini wakati wa mchakato wa kupata wagombea wa chama
hicho.
Wagombea ubunge jimbo la Shinyanga mjini na Solwa Stephen Masele na
Ahmed Salum (kulia) wakifuatilia kwa umakini zaidi hotuba ya mheshimiwa
Mwigulu Nchemba
Mkutani unaendelea
Mheshimiwa Mwigulu Nchemba akimsikiliza mgombea ubunge jimbo la Shinyanga mjini Stephen Masele baada ya kumaliz hotuba yake
Wafuasi wa CCM wakifurahia jambo
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mwanza Anthony Diallo akiwahutubia wakazi wa
Shinyanga leo ambapo alisema Chadema imepoteza mwelekeo kwa kumuweka
Lowassa kuwa mgombea wao huku akisisitiza kuwa Lowassa amenunua Chama
hicho ndiyo maana hata sare za Chama huwa havai kwenye mikutano ya chama
hicho
Tunafuatilia mkutano....
Mkutano unaendelea
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mwanza Anthony Diallo akimnadi mgombea ubunge
jimbo la Shinyanga mjini mheshimiwa Stephen Masele na mgombea udiwani wa
kata ya Ngokolo Emmanuel Mlimandago Dominic
Mkutano unaendelea
Akina mama wakiwa eneo la mkutano
Tunashangilia CCM yetu na wagombea wetu....
Wananchi wakishangilia .....
Mgombea ubunge jimbo la Shinyanga Mjini mheshimiwa Stephen Masele
akiwahutubia wakazi wa Shinyanga ambapo aliwaomba wakazi wa Shinyanga
kumchagua kwa awamu nyingine ili kuinua uchumi katika jimbo hilo.
Wananchi wakimshangilia mbunge wao
"Nipeni muda niwafanyie kazi,ndugu zangu ushabiki hautasaidia,epukeni
kuchagua watu ambao hawana hata anuani...hawajulikani hata wanaishi
wapi...Nimefanya mambo mengi Shinyanga....Nimejenga barabara,nimejenga
hospitali ya rufaa ya mkoa,nimeleta viwanda,katika sekta ya elimu nako
tumefanya makubwa,umeme pia...maji lakini wenzetu hawaoni haya"..alisema
Masele.
Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog
0 maoni:
Post a Comment