
Jiji la kibiashara la Mwanza limejikuta likisimamisha shughuli zake zote
kupisha mkutano mkubwa wa hadhara uliokuwa ukiongozwa na mgombea urais
wa Chadema anayeungwa mkono na vyama vinavyounda umoja wa katiba ya
wananchi UKAWA Edward Lowassa huku zaidi ya wananchi 130 wakizimia.

Kishindo cha mgombea huyo wa nafasi ya
urais Edward Lowassa ndani ya uwanja wa Furahisha kikatikisa afya za
wakazi wa jiji la Mwanza kwa mujibu wa chama cha msalaba mwekundu.
Akiwa jiji Mwanza alikuwa na kazi rahisi zaidi ya kuomba kupigiwa kura
ya ushindi wa kishindo kwakuwa anania, ari na nguvu za kuhakikisha
Tanzania inapata uchumi imara huku akiwataka watanzania kujiandaa vema
na Oct 25 mwaka huu.

Mhe. Edward Ngoyai Lowassa na Highness Kiwia wakiwasili viwanja vya Furahisha Mwanza,leo Jumatatu 12/10/2015


0 maoni:
Post a Comment