TAZAMA BAADHI YA PICHA KATIKA MKUTANO WA AMANI ,MKOANI SHINYANGA!!!

Hapa ni katika ukumbi wa Vigirmark Hotel mjini Shinyanga ambako leo Jumanne,Oktoba 20,2015,wadau mbalimbali wa amani mkoani Shinyanga wamekutana kwa ajili ya majadiliano ya ushirikiano wa kudumisha amani katika kipindi cha uchaguzi mkuu 2015.Kikao hicho kimeandaliwa na uongozi wa mkoa wa Shinyanga likiwemo jeshi la polisi kwa kushirikiana na Shirika la Save The Children linalojihusisha na utetezi wa haki za watoto.

Mambo kadha wa kadha yamejadiliwa ikiwemo kuhakikisha ulinzi na usalama wa watoto kabla,wakati na baada ya uchaguzi,lakini pia viongozi wa vyama vya siasa,wagombea na wanachama kuheshimu na kutekeleza sheria,kanuni,maadili na maelekezo ya tume ya taifa ya uchaguzi pamoja na sheria nyinginezo za nchi katika kipindi chote cha uchaguzi.

Mgeni rasmi katika kikao hicho alikuwa mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Nassoro Rufunga ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama mkoa.

Mgeni rasmi ambaye ni mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Nassoro Rufunga akifungua kikao hicho cha wadau ambapo pamoja na mambo mengine alisisitiza kuwa serikali haiko tayari kuona amani ya nchi inavurugwa hivyo itachukua hatua kali za kisheria kwa watu wote watakaofanya vurugu siku ya uchaguzi.


Mgeni rasmi ambaye ni mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Nassoro Rufunga akizungumza katika kikao hicho ambapo alisema ofisi yake imepata taarifa kuwa kuna baadhi ya wagombea wanatembea na silaha za moto,mapanga,manati na kufundisha vijana mbinu za kuvunja amani siku ya uchaguzi.


Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Nassoro Rufunga akisisitiza kuwa watu wote waliojiandikisha wana haki ya kupiga kura Oktoba 25,2015 na kuwataka baadhi ya watu wanaojipanga kukaa mita 200 kutoka kituo cha kupigia kura kuachana na wazo hilo na badala yake waendelee tu shughuli zao na wakati muda wa kutangazwa matokeo ndiyo warudi vituoni

Wadau wa mkutano huo walisisitiza umuhimu wa wananchi kupiga kura kisha kuendelea na shughuli zao Oktoba 25,2015 badala ya kukaa mita 200/300 kutoka kwenye kituo cha kupigia kura kwa vile kila chama kitakuwa na wakala wake hao ndiyo wataweza kulinda kura zao .Kushoto ni kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga Justus Kamugisha

Wadau wakiwa ukumbini,kulia ni mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro.Wadau wa amani mkoani Shinyanga pia walikubaliana kukabiliana na watu wote wanaopanga kuvuruga amani ya nchi wakati wa uchaguzi. 

Mwakilishi wa shirika la Save the Children Herman Mbunda akizungumzia umuhimu wa kulinda watoto wakati huu wa uchaguzi


Kushoto ni mkuu wa wilaya ya Kishapu Hawa Ng'umbi akiwa na mkuu wa wilaya ya Kahama Vita Kawawa(kulia)

Wadau hao walikumbushana na kuhamasishana kulinda haki za watoto,wanawake na makundi maalum katika jamii wakiwemo walemavu wakati wa uchaguzi 

Kikao kinaendelea


Kikao kinaendelea

Kikao hicho cha wadau wa amani walisema ni vyema katika kipindi hiki cha uchaguzi kila jambo linalofanyika basi kuwe na maslahi kwa watoto ambao asilimia kubwa wanaingizwa katika masuala ya siasa 

Wadau wa amani wakiwa ukumbini

Katibu wa dawati la jinsia kutoka jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga Pili Misungwi(kushoto) akifuatilia kwa umakini zaidi kilichokuwa kinajiri ukumbini

Mkuu wa polisi wilaya ya Shinyanga Richard Ngede(kulia)

Mkutano unaendelea

Kikao cha wadau kinaendelea

Mkutano unaendelea

Wadau wakiwa ukumbini

Viongozi wa dini wakiwa ukumbini


Kikao kinaendelea

Wadau wakifuatilia kilichokuwa kinajiri ukumbini

Kaimu mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Shinyanga Emmanuel Mlimandago(kulia)

Kikao kinaendelea

Kikao kinaendelea


Kikao kinaendelea


Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga Justus Kamugisha akiwasilisha mada ya ulinzi na usalama katika kipindi cha uchaguzi mkuu 2015 ambapo alisisitiza kuwa jeshi la polisi limejipanga vyema kukabiliana na watu watakaovuruga amani ya nchi


Kikao kinaendelea

Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga Justus Kamugisha akizungumza katika kikao hicho ambapo aliwataka waandishi wa habari nchini kutumia vizuri kalamu zao ili kudumisha amani ya nchi

Wadau wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi


Picha ya pamoja washiriki wa kikao hicho


Wadau wakiwa katika picha ya pamoja

Picha ya kumbukumbu

Picha ya kumbukumbu

0 maoni:

Post a Comment