Na Mwandishi wako wa Habari;Yohana Blacklista
WATENGWA ni kundi ama genge la vijana linaloshughulika na muziki wa Hip Hop maarufu zaidi kama ’gangstar rap’ lenye makazi yake jijini Arusha maeneo ya Kijenge.
Kundi hili lilianzishwa miaka 10 iliyopita likiwa na maskani yake kijenge juu, chini ya mtu mzima JCB na Chindo man... kabla ya wao kuanzisha kikundi kwa pamoja waliweza kuanzisha studio yao wenyewe waliyoipa jina la Watengwa Records.
Muvumenti yao hiyo ilileta msisimko mkubwa kila kona ya Jiji la Arusha kwani baada ya watu kusikia kuna studio hiyo ya Hip Hop pale kijenge ya juu basi wasanii wengi wachanga waliweza kufanya ngoma kibao tu.
Kutokana na kuwa na studio yao wenyewe, ndipo mwanamuziki JCB na Chindo waliamua kukaa chini na kutengeneza albamu yao ya kwanza waliyoipa jina la Iliandikwa ambayo albamu hiyo iliweza kuwatangaza vyema Watengwa kama kundi pamoja na studio kwa ujumla. Album hiyo ilibeba nyimbo kama Nawaza, Sina hata taxi, nimefurahishwa na nyingine.
Watengwa iliendeleza harakati zake kwa kuanza kuwatoa wasanii chipukizi (underground) na kuwafanya wajulikanike mitaani kama Donii, Gheto Queen ambaye kwa sasa yupo nchini Marekani katika Jimbo la Califonia... wengine ni D-Wida, Chaba, Boomblast na pia kuna makundi kutoka Moo town (Moshi) yaliweza kufyatua ngoma kibao tu katika studio za Watengwa, makundi hayo ni kama vile Last Society, West Pasu na Mistari team kutoka Pasua Moshi.
Hii ni safari ndefu sana ya Hip Hop kwani kama inavyojulikana album ya kwanza huwa haiachii mikwanja ya kutosha, lakini Watengwa hawakukata tamaa na baddala yake walijipanga na kuweza kuachia ngoma nyingi tu zilizowafanya wajulikane kona zote za Arusha mpaka kufanya hata kwa mtu yeyote anayefika Arusha na kuiulizia Hip Hop basi ni lazima ataambiwa aende kijenge ya juu kwa watengwa.
Mwaka 2005 Watengwa ilipata nguvu zaidi kwa kuongeza memba mpya anayejulikana kama Yuzzo Rubama {ambaye kwa sasa anafanya shughuli zake za kimziki nchini Uholanzi}. Mwaka huo huo (2005) WATENGWA walitoa albam yao ya pili iliyoitwa Full ile Laana ambayo iliwakilisha vizuri sana na kuweza kuiweka juu Arusha kwenye hiphop.
Albam hiyo ya Full ile Laana iliongelea zaidi shida za watu wa mtaa, hasira za vijana na maisha kwa ujumla. Pia walitoa video moja kwenye albam hiyo ambayo ilikua ni Sio lazima ambayo ilichezwa vya kutosha kwenye vituo vya televisheni nyingi za Afrika mashariki. Pia albam hiyo ina vibao kama Nyani, Ukisia Paah {original version}, hatujaja kujaribu na na nyingine kibao tu ambazo nazo zilifanya vizuri sana.
Mwaka uliofata (2006) watengwa ilijijumuisha na wasanii kutoka Kenya, Rwanda na Burundi na kutoa cd ya pamoja ilioitwa East African Up vol.1. Kupitia harakati hizi watengwa ilitambulisha vipaji vingine vipya kama Mapacha, Finger Lou n.k.
Mwishoni mwa mwaka 2007, Watengwa JCB na Chingo walitambulisha albam yao ya tatu waliyoipa jina la Pigo takatifu iliyofanya vizuri katika anga ya muziki wa Tanzania na ilikuwa na vibao kama Tabia mbaya, Wanashangaa, sipotezi muda na ngoma nyingine kibao tu za ukweli ambazo ziliweza kuifanya Watengwa kua nguzo ya Hip Hop Tanzania.
WATENGWA Wakaendeleza harakati hizi kwa kufanya matamasha mbali mbali huku wakipromoti studio na wasanii wao pia. Baada ya muda Chindo na Yuzzo walienda nje ya nchi kutafuta maisha na kuutangaza mziki wao kimataifa zaidi, huku nyuma JCB na Watengwa wengine waliendeleza harakati hapa nchini.
Ndipo JCB alipoamua kutoa albam yake kama solo artist iliyoitwa Nakala za Makalia chini ya produza Daz Maledge ndani ya studio za Watengwa ambapo mpaka sasa albam hiyo ndiyo inayoitambulisha vizuri watengwa na JCB kwa ujumla.
Wakiwa wanakaribia kufikia malengo yao Watengwa wameshusha vifaa vya studio vipya kabisa na vya kisasa zaidi huku wakiwa na waandaaji watatu wa muziki, Simon Fees, D-Wida na Daz Naledge.
Chindo na Yuzzo watarajiwa kurudi Tanzania (Arusha) kwa ajili ya kuzindua upya studio ya Watengwa pia watatumia muda huu kutengeneza albam yao nyingine itakayoitwa Full ile Laana vol.2 ambayo itakua ya kimapinduzi zaidi.
Kwa mtazamo wa JCB amesema albam hiyo itakua ya kiutu uzima zaidi kutokana na ukongwe wao kwenye hii harakati hivyo mashabiki wakae mkao wa kula. Watengwa wanapatikana kwenyewww.myspace.com/watengwa pia wako kwenye page ya facebook kama WATENGWA.
0 maoni:
Post a Comment