
Waziri wa viwanda na biashara ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Handeni
Dr.Abdalah Kigoda amefariki dunia leo majira ya saa 10 jioni nchini
India wakati akiendelea kupatiwa matibabu katika hospitali ya Appolo.
Waziri huyo amefariki dunia wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya Apollo nchini India
Siku chache zilizopita waziri Kigoda alizushiwa kifo katika mitandao ya
kijamii jambo lililokanushwa vikali na serikali kupitia kwa masemaji
wake Bw Assah Mwambene
Dkt Kigoda ni waziri wa pili kufariki
katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu baada ya waziri Celina
Kombani naye kufariki dunia mwezi uliopita katika hospitali hiyo hiyo ya
Apollo ya India alikokuwa akipatiwa matibabu
0 maoni:
Post a Comment