na Yohana Emmanuel
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto, Ummy Mwalimu amesema kuna baadhi ya halmashauri nchini zimekuwa
zikificha taarifa za Kipindupindu kwa kuogopa kuchukuliwa hatua na Rais
Dkt John Magufuli.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu.
“Kuna baadhi ya halmashauri zinaficha taarifa za wagonjwa wa
kipindupindu kwa kuogopa kutumbuliwa na mheshimiwa Rais. Kwasababu
mheshimiwa rais alisema kuwa wakuu wa wilaya na wakurugenzi ambao kwao
kutakuwa na njaa, kipindupindu, atawachukulia hatua. Kwahiyo matokeo
yake watu wamekuwa wakificha taarifa, na inasikitisha sana unakwenda
katika hospitali unakuta wagonjwa wa kipindupindu wamechanganywa na
wagonjwa wengine,” alisema Waziri Ummy wakati akizungumza na waandishi
wa habari kuhusu mlipuko wa ugonjwa wa Kipindupindu katika baadhi ya
maeneo nchini.
“Hili si suala tu la kukiuka maadili lakini ni sawa sawa na mauaji,
ni kosa la jinai, ndio maana kwa kupitia kwenu nawatahadharisha viongozi
wote wa halmshauri kutoa taarifa za wagonjwa wa kipindupindu. Kutoa
taarifa inatusaidia na inasaidia mkoa na halmashauri kuchukua jitihada
mbalimbali za kuchukua hatua,” aliongeza.
0 maoni:
Post a Comment