Msanii wa muziki Bongo, Roma amesema sababu ya baadhi ya wasanii wakongwe kutopenda kuitwa hivyo ni kutokana na kutopewa nafasi katika vyombo vya habari na kuonekana wakati wao umepita.

Roma ameeleza kutokana na hilo wasanii hao wana haki ya kukataa kuitwa wakongwe.
“Unafikiri ishu ni ukongwe, wala si hivyo, ishu ni kuna baadhi ya makundi hayapewi nafasi kwenye media house, mchongo ndio upo hapo, hizo nyingine zote mchongoma tu,” amesema.
“Snoop Dog ni mzee anafanya mchongo na Wiz Khalifa, kwanini Mox asifanye mchongo na Country Boy halafu ukawa kweli mchongo lakini sisi tunakuja kuitafsiri mkongwe hana nafasi kwenye generation ya sasa hivi which is total wrong,” ameongeza.
Ameendelea kwa kusema ikiwa msanii ataitwa mkongwe lakini anapata kile ambacho anastahili wala hakuna ambaye angelaumu ila kwa namna inavyotafsiriwa na watu wa vyombo vya habari sivyo.
Klabu ya soka ya Mbao FC, imetangaza rasmi kumsajili kocha Amri Said.


























Kocha huyo amesaini mkataba wa miaka minne ambao utamalizika msimu wa mwaka 2021/2022. Makubaliano hayo yamefikiwa katika ofisi za makao makuu ya wadhamini wa Mbao, GF Trucks &Equipment ltd zilizopo Vingunguti jijini Dar es salaam.
Msimu uliopita Amri Said alikuwa akiifundisha Lipuli FC huku msaidizi wake akiwa Selemani Matola na kuisaidia timu hiyo ikimaliza ligi kuu ikiwa kwenye nafasi ya saba.
Wakati huo huo Mbao imenusurika kushuka daraja msimu ulioisha ikiwa nafasi ya 14 na huku ikiambulia alama 29.
Msanii wa muziki nchini Nigeria, Yemi Alade amejikuta na hali ya taharuki akiwa location baada ya askari polisi mjini Lagos  kumtawanya yeye na madensa wake kwa kupiga risasi za moto angani.

Yemi Alade kupitia ukurasa wake wa Twitter amesema kuwa wakati akiwa location katika mitaa ya Ikeja ku-shoot video ya wimbo wake mpya alishangaa kuona askari kanzu (askari upelelezi) wakikoki bunduki na kufyatua risasi angani bila hata sababu maalumu.
Mkali huyo wa Hit ya Johnny, amesema kuwa askari waliokuwa umbali wa mita 10 walimsogelea na kumwambia kuwa wamesikia eneo hilo kuna vurugu na kuwaamuru watawanyike upesi bila shurti.
“Sigh…So Here i am jejely giving them some mad dance moves on set of a Video shoot somewhere in Ikeja and a uniformed officer pulls his trigger for no reason 10 steps from where i stood and puts everybody in panic mode! This man said he heard people were fighting!! Lets not even talk about the egotistic air head that was granted VIP protection from the police (he probably told the policeman to announce his presence with a gun shot). To think that My entire team.stood right next to him!what if the bullet hit someone! You mean in a peaceful gathering where “lazy nigerian youths” are trying to make a living ,the only way to announce your uninvited self is to shoot for no reason!”
Hata hivyo, Yemi Alade amelishukia jeshi hilo la polisi kwa kudai kuwa wanatumia ovyo kodi za wananchi kwa kutumia risasi maeneo ambayo hayastahili.
“Do you know how expensive bullets are? You make us pay tax then use tax payers money to buy bullets and arms so you can shoot tax payers. We need to curb This disregard for human life in Nigeria! Do human rights even exist here!?Is justice never going to be an action word!”
Kwa mujibu wa mtandao wa Nigeria NewsDesk umeeleza kuwa Yemi Alade hakuwa na kibali maalumu cha ku-shoot video katika eneo hilo alilotawanywa na polisi.
Rais wa Nigeria, Muhammadu Buhari mwaka jana alitangaza kuwa vijana wengi wa Nigeria hawafanikiwi kwa sababu ni wazembe, hawajitumi na wanapenda starehe ndio maana Yemi Alade ametumia Hashtag ya#lazynigerianyouths ambayo ilitumiwa na mastaa kibao nchini humo mwaka jana kumpinga rais Buhari.
Msanii wa Bongo Flava kutoka Mdee Music, Mimi Mars amefunguka iwapo yeye na Vanessa Mdee kuna siku wataingia rasmi katika muziki wa Injili.

Utakumbuka Mimi Mars pamoja na Vanessa Mdee wameshirikishwa na dada yao, Nancy Hebron ambaye anafanya muziki wa Injili katika wimbo wake uitwao Beauty Jesus.

Muimbaji huyo ameiambia Bongo5 kuwa walishiriki katika wimbo huo kwani waliombwa kufanya hivyo ila haimanishi kuwa wana mpango wa kuingia huko moja kwa moja.

“Hapana, Nancy ni mtu ambaye ni ndugu yetu na ameingia kwenye muziki hivi karibuni na aliomba sana tufanye naye wimbo wa gospel, kwa hiyo tukaona si vibaya ingawa tunafanya muziki wa dunia pia tunamwabudu Mungu, tunaenda kanisani,” amesema.
“Sio kwamba namaanisha tunaingia kule, hapana!, lakini ilikuwa ni kum-support na kuonyesha watu tupo hata kwenye suala la dini,” ameongeza.
Tangu kuingia kwake rasmi kwenye Bongo Flava mwaka jana na kuachana na kazi ya utangazaji, Mimi Mars ameweza kutoa nyimbo nne ambazo ni Sugar, Dede, Sitamani, Papara pamoja na kufanya kolabo kadhaa.
Hakuna asiyefahamu uwezo mkubwa wa muimbaji Ruby, lakini kila mmoja amekuwa akishangaa ni kwanini mrembo huyo anashindwa kwenda mbele zaidi kimuziki kutokana na kipaji chake cha asili kilichopo ndani yake.

                                                          
 Ruby
Mrembo huyo ambaye ni zao la Serengeti Super Nyota 2014, aliwahi kufanya kazi na THT chini ya Ruge Mutahaba wa Clouds Media na kupata mafanikio makubwa sana kwa muda mfupi kupitia wimbo wake ‘Na Yule’ambao uliteka vyombo vya habari.
Hata hivyo hakukaa muda mrefu aliachana na uongozi huo kwa kashfa nyingi na kuamua kujisimamia mwenyewe lakini hakuweza kufanikiwa kwani kila siku zilivyozidi kwenda aliendelea kupotea taratibu huku mashabiki wakijiuliza kitu gani kinamsumbua binti hiyo.
Mwezi huu amerudi umpya na wimbo ‘Niwaze’ ambao unaonekana kuwavutia watu wengi huku wadau wakidai huwenda pia ni kutokana na ukimya wake wa muda mrefu.
Jumatatu hii mrembo huyo amedai ameachana na ‘umapepe’ kitu ambacho kilikuwa kikitajwa na watu wengi hasahasa wadau wa muziki kwamba ndio kinachomkwamisha mrembo huyo.
“Umapepe nishatupa kuleeekuleee😂🙈💃tangu enzi za….💃😘niambie na ww mstari upi unakubamba😍,” Ruby alitoa ujumbe huo kupitia Instagram.
Kwa sasa muimbaji huyo hajaweka wazi anafanya kazi chini ya label gani lakini aliahidi mambo yakikaa sawa ataweka wazi kila kitu.
Wewe kama shabiki wa muziki na mdau unadhani mrembo huyo alikuwa anasumbuliwa na ‘umapepe’ au ana kitu kingine cha ziada kinamsumbua?. Toa maoni yako hapa chini au kipitia mitandao yetu ya kijamii.

Hit maker wa ‘Sina Jambo’ Bill Nass au Bill Nenga amehitimu rasmi masomo yake katika Chuo cha Biashara (CBE) kilichopo jijini Dar Es Salaam, na kutunikiwa Shahada yake ya kwanza.
Rapper huyo wa ngoma kadhaa zinazofanya vizuri katika media mbalimbali ameingia katika orodha ya wasanii waliohitimu masomo yao kwa mwaka huu kama vile mkali wa RnB Bongo, Jux aliyehitimu masomo yake mwaka huu nchini China.
Pia atakuwa mwiongoni mwa wasanii mwenye elimu ya juu ambao kuna mastaa kama  katika kiwanda cha burudani nchini .
Majina matano ya wanasoka wanaowania tuzo ya BBC ya mchezaji bora barani Afrika yametajwa ambapo wachezaji kutoka Ligi kuu England wameendelea kumiliki orodha hiyo tangu tuzo hizo zianze kutangazwa. Ambapo klabu ya Liverpool imetoa wachezaji wawili mwaka huu Sadio Mane na Mohamed Salah.
Majina ya wachezaji hao watano ni Pierre-Emerick Aubameyang, Naby Keita, Sadio Mane, Victor Moses na Mohamed Salah.
Jopo la wataalamu na wakongwe wa soka ambalo liliundwa na Emmanuel Amuneke, mshindi wa ubingwa Afrika na Olimpiki 1996, Arnaud Djoum, mshindi wa Kombe la Mataifa ya Afrika 2017 akiwa na Cameroon, na Jean Sseninde, kutoka Uganda anayechezea Crystal Palace Ladies, walikuwepo kujadili majina ya wachezaji walioteuliwa kushindania tuzo hiyo.
Hata hivyo mshindi wa tuzo hiyo wa mwaka jana, Riyad Mahrez anayekipiga kunako klabu ya Leicester City na timu ya taifa ya Algeria hajatajwa mwaka huu.
1-Naby Keita – RB Leipzig na Guinea
Tokeo la picha la Naby Keita
Naby Keita amekuwa gumzo nchini Ujerumani kutokana na kiwango alichokionesha akiwa na klabu ya Rb Leizpg na msimu huu alitajwa katika kikosi bora cha Bundesliga.
Klabu ya Red Bull Leipzig iliwashangaza watu wengi katika msimu wa 2016-17, huku ikimaliza katika nafasi ya pili (na kufuzu katika mashindano ya vilabu bingwa), lakini ilikuwa kiungo huyo wa kati aliyeisadia timu hiyo kumaliza katika nafasi ya pili.
Kwa jumla, alifunga mabao manane, mojawapo likiwa bao lililoorodheshwa kuwania tuzo ya bao bora la msimu huku akitoa usaidizi katika ufungaji wa mabao 7.
2-Pierre-Emerick Aubameyang – Gabon na Borussia Dortmund
Tokeo la picha la Pierre-Emerick Aubameyang 
Msimu uliopita alifanya makubwa Ujerumani akifunga mabao 35 na kuweka rekodi kuwa mchezaji wa 4 kuwahi kufunga mabao 30 nchini Ujerumani huku akiwa Muafrika wa kwanza kufikisha mabao hayo katika Bundesliga.
3-Sadio Mane –Senegal & Liverpool
Tokeo la picha la Sadio Mane
Alikuwepo katika kikosi cha Epl cha waandishi wa habari za michezo, alichaguliwa mchezaji bora wa klabu ya Liverpool msimu uliopita huku pia hapo jana akiisaidia Senegal kufuzu kwa fainali za kombe la dunia kwa kuichapa Afrika Kusini.
4-Mohamed Salah –Egypt & Liverpool
Tokeo la picha la mohamed salah
Ameiwezesha Misri kushiriki michuano ya kombe la dunia lakini msimu uliopita alikuwa na kiwango kizuri sana alipokuwa Fiorentina huku msimu huu akiwa amefunga mabao 7 katika ligi ya Epl.
Victor Moses –Nigeria na Chelsea
Tokeo la picha la victor moses
Kama ilivyo kwa Salah na Mane huyu naye tayari timu yake imefuzu kuelekea Urusi, Victor Moses tangu kocha Antonio Conte ajiunge na Chelsea amekuwa akimpa sana nafasi japokuwa msimu huu ameandamwa na majeraha yanayomuweka nje hadi sasa.
Kwa Mama ana yenyonyesha ni kawaida kupungukiwa na maziwa pindi akiwa ananyonyesha hasa baada ya kujifungua.
Baadhi ya wamama wamekuwa wakikata tamaa namana ya kuweza kuongeza maziwa ili waweze kunyonyesha. Na wengine huamua kutumia maziwa ya kopo au maziwa ya ng’ombe kwa mtoto.(watoto)
Baadhi ya njia zinazoweza kusaidia kuongeza mama maziwa.
i). Uji wa pilipili manga-utapika ujimwepesi changanya na pilipili manga ,kunywa mara 2 kwa siku asubuhi na jioni.
ii). Mbegu za maboga-unaweza zitafuta au kuchanganya kwenye uji au chai.
iii). Juice ya karoti changanya na tangawizi kunywa mara 2 kwa siku.
iv). Supu ya samaki au nyama iliochanganywa na mboga mboga kunywa mara 1 kwa siku.
v). Maji ya kunywa ni muhimu zaidi kunywa kwa wingi .
Chanzo: Mtandao
Huenda siku za usoni tukasahau kabisa kama kulikuwa na kundi la muziki la P-Square kwani kwa sasa mapacha hao wanaanza kuuza baadhi ya assert zao ambazo walikuwa wanamiliki wote kwa pamoja kipindi wakifanya muziki kama kundi, Baada ya taarifa kusambaa kuwa wawili hao wanapiga mnada jumba lao la kifahari lililopo jijini Lagos, Nigeria.
Square Ville
Taarifa kutoka kwenye vyombo vya habari  nchini Nigeria zinaeleza kuwa wawili hao wamefikia hatua ya kupiga mnada nyumba hiyo iliyopo eneo la Ikeja, jijini Lagos ili kila mmoja aweze kumiliki vitu vyake na hii inakuwa ni hatua ya kwanza tangu watangaze kundi hilo kusambaratika.
Nyumba hiyo ya kifahari waliyoipa jina la ‘SquareVille’ inauzwa kwa Naira milioni 320 sawa na bilioni 2 za kitanzania.
Tayari jumba hilo limeshawekwa lebo ya kuuzwa mbele ya geti tangia jumatano ya wiki hii ingawaje mpaka sasa wahusika wamegoma kuzungumzia ishu hiyo lakini kampuni LIB ambayo ndiyo inahusika na upigaji mnada wa nyumba hiyo imethibitisha hilo.
Nyumba hiyo ambayo ina vyumba 16 na swimming Pool ilijengwa mwaka 2010 ambapo kundi hilo lilitangaza wazi kuwa kiwanja tu cha mjengo huo kiliwagharimu Naira milioni 100.
Serikali imetakiwa kutoa tamko ambalo litakuwa ni hatma kwa wanafunzi wa vyuo vikuu waliokosa mkopo kutokana na sababu mbalimbali.


Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Idara ya Haki wa Mtandao wa wanafunzi Tanzania Bw. Abdul Omary Nondo alipokuwa akiongea na waandishi wa habari mapema leo jijini Dar es salaam.

Mkurugenzi huyo aliendelea kwa kusema kuwa wanafunzi waliotakiwa kupatiwa mikopo ni 61 elfu na badala yake wamepatiwa 30 elfu peke yake na katika hao walioachwa kuna yatima na wengine wasio na uwezo wa kumudu gharama hizo zote.


Katika Mkutano Mkuu wa wadau wa TAMSYA, uliofanyika leo Novemba 12 jijini Dar es Salaam, vijana wa kiislamu wahimizwa kuwa na umoja katika jamii.
Hayo yamebainishwa na wadau mbalimbali akiwemo Rais wa Taasisi hiyo, Ramadhani Ulende ambapo amewataka vijana wa kiislamu kuwa na umoja ili kuimarisha moja ya dhumuni la kuanzishwa kwa Taasisi hiyo.
Pia kiongozi huyo amebainisha kazi mbalimbali wanazofanya ikiwemo kusaidia vijana na wanafunzi nchini kote na kueleza kuwa moja ya malengo ni kutatua changamoto zinazowakabili wanafunzi na vijana kwa ujumla.
Vile vile kiongozi huyo ametoa wito kwa taasisi zingine kujumuika kufanya kazi nao huku akitaja kuwa wao wekuwa wakifanya kazi kwa kuwajengea uwezo vijana kwa kwa kuwapatia mafunzo mbalimbali ya ujasiliamaji na kuwapatia msaada wa kimawazo.
Kwa upande wa Mlezi wa Jumuiya hiyo kwa Mkoa wa Dar Es Salaam, Mzee Issa amesisitiza wanajumuiy hiyo kuwa na undugu, kuwa na mahusiano mazuri yatakayoweza kuwa tija kwa jamii hii ni pamoja na kuhakikisha wanapambana katika kutafuta miradi itakayo weza kutoa ajira.
TAMSYA ni kirefu cha neno Tanzania Muslim Student and Youth Association, ilianzishwa mwaka 1993 na ilifahamika kama TAMSA.
Mnamo mwaka 2010, tarehe 13 mwezi 10 jina la TAMSA lilibadilishwa na kuwa TAMSYA yenye lengo la kuwasaidia vijana na wanafunzi wa kiisalamu katika kutatua changamoto mbalimbali ikiwemo za kimaisha.
Pia TAMSYA imekuwa ikifanya kazi ya kuwapa misaada wanafunzi wenye uhitaji wa kupata elimu ya juu kwa kuwaombea nafasi za masomo au kuwaunganisha na sekta husika pamoja na kuwatengenezea njia.
Kikosi cha Mpira wa Kikapu cha Muembetanga Kikichokubali kipigi cha Vikapou 131 - 38 katika mchezo wake wa Ligi Kuu ya Kikapu Kanda ya Unguja michezo inayofanyika katika Uwanja wa Gymkhana, kutafuta Bingwa wa Mchezo huo kushiriki Ligi Kuu ya Muungano Mpira wa Kikapu Tanzania. 
Mchezaji wa Timu ya Muembetanga akijaribi kuziiya mpira ukielekea katika wavu wakati wa mchezo wa Ligi Kuu Mpira wa Kikapu Kanda ya Unguja mchezo uliofanyika Uwanja wa Gymkhana Timu ya Stone Town imeshinda kwa Vikapu 131 0 38.
Mchezaji wa Timu ya Stone Town Saidi Marini akijiandaa kumpita mchezajhi wa Timu ya Muembetanga wakati wa mchezo huo uliofanyika uwanja wa Gymkhana Timu ya Stone Town imeshinda kwa Vikapu 131 - 38. 







Je, wewe ni mmoja ya watu wanaohangaika kulipa madeni? basi ni mmoja wao ni vyema ukajitahidi kulipa madeni hayo kwani utafiti unaonesha kuwa watu wanaohangaika au kushindwa kulipa madeni wapo hatarini zaidi kukumbwa na magonjwa ya moyo ukiwemo ugonjwa wa shambulizi la moyo (Heart Attack).
Utafiti huo uliofanywa na wasomi kutoka katika chuo kikuu cha Witwatersrand cha nchini Afrika Kusini wamesema watu wengi wanaohangaika kulipa madeni wapo kwenye hatari ya kupatwa na maradhi ya moyo mara 13 ya watu wanaohangaika kutafuta kazi na wale wenye changamoto kwenye sehemu zao za kazi.
Utafiti huo uliyoongozwa na Dkt. Denishan Govender umeonesha kuwa watu wengi wenye madeni hukosa usingizi na muda mwingine hukosa amani kila wanapokumbuka madeni kitu ambacho kinawafanya wakose amani muda wote.
Dkt. Denishan Govender amesema walichukua idadi ya wagonjwa 106 wanaougua ugonjwa wa Shambulio la Moyo, ambapo wagonjwa 96 kati ya hao wamesema kuwa walikuwa wamepatwa na msongo wa mawazo kwa madeni na majukumu ya kifamilia.
Tulichogundua ni kwamba watu wengi wanapoenda hospitalini wanaulizwa vitu tofauti na madaktari kwani maswali yao utasikia unatumia sigara? au unatumia pombe au unalala muda gani? kumbe hiyo huenda isiwe sababu ya moja kwa moja.“amesema Dkt. Govender kwenye kongamano kubwa linaloandaliwa kila mwaka nchini Afrika Kusini maalumu kwa kutoa elimu ya afya ya moyo.
Wagonjwa wengi wanashauriwa kupunguza msongo wa mawazo kwa kufanya mazoezi ila fikiria kwa nini magonjwa ya moyo kama Shambulizi la Moyo hayapungui? hapa kuna sababu kama hizo za kiuchumi ambapo hata kama mgonjwa akifanya mazoezi wiki nzima bado hawezi kusahau madeni au majukumu mengine yanayohitaji fedha kuna vitu vimebadilika kwa dunia ya sasa.“amesema Dkt. Govender.
Hata hivyo, Dkt. Govender amesema kuwa watu wengi magonjwa ya moyo huwapata pale wanapoanzia utotoni lakini dalili zake huanza kuonekana kadri umri unavyozidi kuogezeka.
Kwenye utafiti huo umeonesha kuwa mabadiliko ya kiuchumi na aina ya vyakula ndio vyanzo vikubwa vya magonjwa ya moyo. Pengine kuliko hata matumizi ya sigara au pombe.

Polisi mkoani Morogoro imefanikiwa kumtia mbaroni Nehemia Nashoni kwa tuhuma ya kukutwa akiwa na pembe za ndovu vipande vitano yenye thamani ya zaidi ya Sh milioni 100 kwenye nyumba ya kulala wageni ya B-Z iliyopo Nane Nane, Manispaa ya Morogoro.


Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro, Ulrich Matei alisema jana kuwa tukio hilo lilitokea Novemba 8, mwaka huu saa nne usiku maeneo ya Nane Nane katika Hoteli ya B-Z iliyopo Manispaa ya Morogoro.

Alisema kuwa, askari Polisi wakiwa doria walipokea taarifa za kuwepo kwa mtu mmoja aitwaye Nehemia Nashoni akiwa na pembe za ndovu na kufanikiwa kumkamata. Kamanda huyo wa Polisi wa Mkoa alisema, baada ya kumpekua alikutwa akiwa na pembe za ndovu vipande vitano vyenye uzito wa kilo 20 katika chumba namba 104 alichokuwa amekodi katika hoteli hiyo.

Kwa mujibu wa Kamanda huyo thamani za pembe hizo ni zaidi ya Sh milioni 100. Kamanda Matei alisema kuwa hatua zinazofuata ni za kumfikisha mahakamani mtuhumiwa huyo na alitoa wito kwa wananchi wa Morogoro kuendelea kushirikiana na Polisi katika kuwafichua wahalifu na uhalifu. 

HATIMAYE serikali imetoa vigezo vinavyotakiwa kutumika kama vipaumbele wakati wa kuwapandisha watumishi wa umma mshahara.

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dk Laurean Ndumbaro ndiye aliyetangaza vigezo hivyo vinavyopaswa kutumiwa na waajiri katika utumishi wa umma kuwapandisha watumishi mishahara.


Kwa mujibu wa Katibu Mkuu Ndumbaro, suala la upandishwaji vyeo kwa watumishi wa umma litazingatia zaidi utendaji kazi wa mtumishi husika na si suala la sifa ya Muundo wa Utumishi (Scheme of Service) pekee kwa maana ya muda wa kutumikia miaka mitatu mitatu kama wengi wanavyodhani.

Aliyasema hayo kwa wakati tofauti katika Halmashauri za Wilaya ya Nyasa, Namtumbo na Manispaa ya Songea katika ziara yake ya kikazi ya siku tano ya kuhimiza uwajibikaji mkoani Ruvuma.

Katibu Mkuu Ndumbaro alisisitiza kuwa mtumishi wa umma anayewajibika vizuri katika utendaji kazi wake wa kila siku ndiye atakayepandishwa cheo na si vinginevyo. 

Alilazimika kutoka ufafanuzi huo, kufuatia baadhi ya watumishi katika halmashauri hizo kulalamika kutopandishwa madaraja (vyeo) kwa wakati kwa muda mrefu sasa wakati wenzao walioanza nao kazi wameshapandishwa vyeo, hivyo kusababisha uwepo wa tofauti kubwa ya mishahara baina yao.

“Haiwezekani Serikali ikapandisha mishahara kwa watumishi wasiowajibika, walevi na wasio na nidhamu na uadilifu katika utendaji wao wa kazi, atakayewajibika katika utendaji wake ndiye atakayepandishwa ngazi ya mshahara,” alisisitiza.

Katibu Mkuu huyo aliainisha kuwa, malalamiko mengi ni ya walimu ambao wamekuwa wakidhani kuwa kila baada ya miaka mitatu lazima wote wapandishwe vyeo (madaraja) hata kama hawajawajibika ipasavyo, suala ambalo si sahihi.

“Haiwezekani Mwalimu anayefundisha vizuri darasani na wanafunzi wake wanafaulu vizuri masomo yake akapandishwa daraja sawasawa na yule ambaye ufundishaji wake hauridhishi na ni mlevi wa kupindukia hali inayochangia wanafunzi wengi kutofaulu somo lake.”

Aidha alisema hivi karibuni, ofisi yake inatarajia kukutana na Tume ya Utumishi wa Walimu na kuzungumza na Walimu ili kutoa elimu na ufafanuzi yakinifu wa vigezo vya msingi vinavyozingatiwa katika suala la upandishaji vyeo kwa watumishi wa umma nchini kwa lengo la kuepukana na malalamiko yasiyo ya lazima.
Askofu mstaafu wa kanisa la Pentekoste (FPCT)  Singida mjini Dk. Paul Samweli, amesema suala la serikali ya Dk.  John Magufuli kusisitiza ulipaji wa kodi na ushuru ni ulekezaji wa maagizo ya Yesu Kristo,  hivyo waumini na Watanzania kwa ujumla, wanatakiwa kutii na kuzingatia wajibu wao huo.
Akiijengea nguvu hoja yake hiyo, amesema kwa mujibu wa kitabu kitakatifu cha Mungu  cha biblia Warumi 13  (msitari 1-14), inaonesha wazi Yesu kristo alipigia debe Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA). 
Askofu Paul alisema katika Warumi 13  kimeainisha kuwa watoza kodi na ushuru, ni wahudumu wa Mungu kuwa wapeni haki zao, mtu wa kodi, kodi, mtu wa ushuru, ushuru.
Dk. Paul amesema hayo juzi wakati akihubiri kwenye ibada ya kawaida ambayo pia ilihudhuriwa kamanda wa jeshi la polisi  mkoa mkoani  hapa ACP Debora Daudi Magiligimba.
Akisisitiza, alisema kwa vile ulipaji   kodi umepewa baraka zote na Mwenyezi Mungu, waumini wa madhehebu mbalimbali ya dini, wanapaswa kuwa mstari wa mbele katika kutii agizo la Mungu la kulipa kodi uliowekwa kisheria bila shurti.
“Serikali ya Rais Magufuli katika hili la uhimizaji wa ulipaji kodi na ushuru, inafanya vizuri kazi iliyopo mbele yetu waumini wa dini na Watanzania kwa ujumla, ni kulipa kodi na ushuru kwa wakati, ili nchi yetu iweze kusonga mbele kimaendeleo. Haya mambo ya  kukwepa kulipa kodi au ushuru, yakomeshwe,” alisema.
Kuhusu watoza kodi na ushuru Dk.Paul, alisema kuwa katika Biblia (Luka Mtakatifu 3 -12-17)  inasema  watoza kodi/ushuru waliagizwa wasitoze kubwa ambayo itakuwa kinyume na sheria inavyoagiza.
Alifafanua, alisema wafanyakazi wa TRA, katika utekelezaji wa majukumu yao, wanatakiwa kutoza kodi na ushuru kwa mujibu na sheria, kanuni na taratibu zilizowekwa na si vinginevyo.
“Wakitoza kodi au ushuru mkubwa ambao upo  kinyume na sheria, watakuwa wanamudhulumu mlipaji, kitendo hicho sio tu binadamu mwenye maadili mema hakipendi, lakini pia, nacho hakitampendeza Mwenyezi Mungu,” alisema.
Kwaupande wa jeshi la polisi, Dk. Paul amesema kwamba katika kitabu cha Warumi 3 mstari wa 14, kimewataka askari polisi katika kutekeleza majukumu yao, wasidhulumu mtu wala wasiwababikizie watu kesi za uongo. Pia watosheke na mshahara wanaolipwa.
“Kamanda maneno yaliyotamkwa  na mtumishi wa Mungu Yohana, yanamtaka  kila askari polisi, aridhike na mshahara wake. Ina maana asiwe na tamaa ya kuomba rushwa na vile vile asibabikie  mwananchi kesi, bali atatekeleza wajibu wake kwa mujibu wa mkataba wake wa kazi,” alisema.
Dk. Paul alitumia  fursa hiyo kulipongeza jeshi la polisi mkoa wa Singida kwa juhudi zake za kudhibiti vitendo vya kihalifu ambavyo vinaweza kuhatalisha amani na utulivu ulipo.
“Nikupongeze kipekee kamanda Magiligimba kwa kuazisha utamaduni mpya wa kuongea na waumini wa madhehebu ya dini kwenye nyumba zao ibada. Pia kwa uamuzi wako wa kudhibiti uhalifu kabla haujatokea. Kwa kifupi unataka dalili za kutokea uhalifu, zishughulikiwe mapema kabla hazijaleta madhara. Sisi kanisa tunakuunga mkono katika hili. Mungu akutangulie,” alisema Dk.Paul.