Pazia la wansiasa watanaotaka Urais ndani ya chama cha Mapinduzi limefunguliwa mwezi huu mkoani Dodoma ambapo wimbi la makada wa chama hicho wamemiminika kuchukua fomu za kuomba ridhaa ya kuteuliwa kugombea urais.
Hadi sasa wanasiasa takribani wanasiasa 27 huku wengine wakiongezeka wamechukua fomu wakiwemo hawa wafuatao; Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa, Waziri wa Uchukuzi, Samuel Sitta, Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Steven Wasira, Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki, Makongoro Nyerere, Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye, Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Dk. Titus Kamani, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Kazi Maalumu) Profesa Mark Mwandosya.
Wengine ni Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli, Aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba, Balozi Ali Karume, Amosi Siyantemi, Balozi Amina Salim Ali na Makamu wa Rais Dk. Gharib Mohammed Bilal.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, Mbunge wa Kisesa Luhaga Mpina, Mwele Malecela, Mbunge wa Nzega, Dk. Hamis Kigwangalla, Waziri wa Maliasilia na Utalii, Lazaro Nyalandu, Peter Nyalali, Leonce Mulenda na Musa Mwapango, Waziri wa Mambo ya Ndani, Mathias Chikawe, Eldefonce Bilohe, Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja, Naibu Waziri wa Mawasiliano Sayansi na Teknolojia, Dk. KitineBoniface Ndengo na Boniface Ndengo.
Kila mwanasiasa aliyetangaza nia amekuja na sera pamoja na vipaumbele vyake ikiwa atapata kuteuliwa kushika wadhifa huo mkubwa katika uongozi wenye misingi ya Demokrasia hapa nchini.
Baadhi ya sera na Vipaumbele hivyo ni kukabiliana na hali duni ya Maisha huku kukiwa na utofauti mkubwa kati ya wenye nacho na wasio nacho, kupambana na Rushwa na Ufisadi, kuimarisha Muungano, kuboresha miundombinu pamoja na wengine kujinadi kuwa watachukua maamuzi magumu.
Aidha,wanasiasa hao hakuna aliyethubutu kuweka sera imara ya kukabiliana na mauaji ya Albino yaliyozuka nchini Tanzania hasa katika maeneo ya Kanda kwa imani za kishirikina huku baadhi ya watu wakidhani viungo hivyo vinaleta utajiri.
Baadhi ya Wanasiasa akiwemo Mbunge wa Monduli Edward Lowassa aligusia kuwa akiteuliwa kuwa rais atapambana suala la mauaji ya Watu wenye Ulemavu wa Ngozi(albino) pasipo kuweka katika moja ya vipaumbele vyake na kushindwa kutaja mbinu na mikakati ya jinsi ya kukabiliana au kumaliza kabisa suala la mauaji hayo linalochafua jina na suara ya Tanzania kimataifa.
Wakizungumza na Mwandishi wa Hivisasa baadhi ya watu wenye ulemavu wa Ngozi mkoani Dodoma,Mwanza na Simiyu wamekiri kuwa hadi sasa hakuna Mtangaza nia ata mmoja aliyeweza kuweka mikakati thibiti kumaliza tatizo la mauji ya Albino suala linalopelekea wao kukosa imani na wagombea hao endapo wakipewa ridhaa ya kuiongoza Tanzania.
Mmoja kati ya hao ni Asumta kutoka mkoani Mwanza amesema kwamba Mwanasiasa ambaye angeweka mikakati thabiti ya kukabiliana na tatizo la Mauaji hayo basi angejizolea kura zote kutoka kwa watu wenye ulemavu wa ngozi nchini.
Ameongeza kuwa wanasaiasa hao wamejaribu kugusia kidogo kukabaliana na janga hilo lakini hata hivyo haitoshi kuwashawishi wao kuamini kuwa watakabiliana na tatizo ya mauaji ya watu wenye ualbino nchi kwa kuwa bado wana ishi wa hofu ndani ya nchi yao inayodaiwa kuwa ni kisiwa cha amani.
Kwa upande mmoja wa aliyewahi kuwa kiongozi wa chama cha watu wenye ualbino kutoka kanda ya Ziwa amesema kwamba asilimia kubwa ya watangaza nia wanawaza kuingia Ikulu ndio maana mauaji ya watu wenye ualbino siyo ajenda kwao.
Ipo haja ya wanasiasa waonataka kuingia Ikulu kuweka moja ya sera zao ni suala la mauaji ya albino ili watu wenye ualbino waweze kuishi kwa amani ndani ya nchi yao kwa suala la mauaji ya albino bado halijapata ufumbuzi wa kudumu licha ya serikali kuweka mikakati mbalimbali ikiwemo kifungo cha maisha kwa baadhi ya watuhumiwa waliokamatwa kwa tuhuma za kuhusika moja kwa moja na mauaji hayo.
Takwimu za kutoka mwaka 2006 zinaonyesha kuwa Albino 74 wameshauawa kikatili, huku 56 wakinusurika kifo, na kati yao 11 wameongezewa ulemavu mwingine wa kudumu.
0 maoni:
Post a Comment