MKULIMA ALIYECHUKUA FOMU YA KUGOMBEA URAISI 2015


Mkulima Bw. Idelphonce Bilole akizungumza jambo na Waandishi wa Habari mara baada ya kuchukua fomu.
Mkulima Bw. Idelphonce Bilole akizungumza jambo na Waandishi wa Habari mara baada ya kuchukua fomu.
Mkulima wa darasa la saba achukua fomu rasmi za kugombea urais,
Mkulima wa darasa la saba achukua fomu rasmi za kugombea urais,
Mkulima aliyechukua fomu ya kugombea urais ajulikanaye kama Idelphonce Bilole amewasili mkoani Morogoro jana  kusaka wadhamini ikiwa ni moja ya masharti ya jumla kwa wagombea urais wote ambapo wanatakiwa kuwa na wadhamini kutoka mikoa 15 nchini.
Mkulima huyo  katika safari yake ya kuingia Ikulu ana falsafa ya  elimu si kigezo cha yeye kushindwa kuwania nafasi hiyo ya juu na kujitapa kuwashinda wanasiasa wakongwe akiwemo Mbunge wa Monduli Edward Lowassa pamoja na Bernad Membe.
Akizungumza katika  katika ofisi ya CCM Wilaya ya Morogoro  amesema Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inasema kiongozi ni lazima ajue kusoma na kuandika na kwamba CCM ni chama pekee ambacho hakina ubaguzi.
Katika suala liliwashangaza wengi Mkulima huyo amesema na eye pia ni mmoja kati ya watu walioshawishiwa kugombea urais hapa nchini huku akisisitiza kuwa  mwaka 2003 alifuatwa na baadhi ya viongozi wa chama hicho wakimtaka ajiandae ili aweze kuwania nafasi hiyo.
Hivyo basi  mwaka 2005  amesema alikubali na aliandika barua ya kuomba kuteuliwa, lakini kutokana na sababu ambazo yeye hakuzifahamu barua ile ilichelewa na hivyo kuamua kuvuta subira hadi mwaka 2015 alipo amua kuvunja ukimya.
Hadi sasa mkulima huyo ameshapata wadhamini  katika mikoa kadhaa ikiwemo Dodoma, Kigoma, Mwanza, Simiyu, Singida, Shinyanga, Geita na  Morogoro.
Ameongoza kuwa  mwaka huu ameona ni muda muafaka wa yeye kuwania nafasi hiyo ambayo wanachama wenzake wamekuwa wakimuomba kugombea kwa muda mrefu.

0 maoni:

Post a Comment