Hatimae bunge limepitisha bajeti ya serikali ya shilingi trilioni 22.495 kwa mwaka wa fedha 2015/16 ikiwa na ongezeko la tozo ya shilingi 100 kwa mafuta kila lita ya mafuta ya Taa, Petroli na Dizeli, licha ya jitihada za baadhi ya wabunge kutaka serikali kupunguza hizo ili isiwaumize watu wa kipato cha chini.
Akijibu hoja za wabunge zilizotolewa katika mjadala ya bajeti hiyo, waziri wa fedha na uchumi Mhe Saada Mkuya amesema tozo hiyo itasaidia kuingozea mapato ya serikali ya shilingi bilioni 276 ambapo kati ya fedha hizi shilingi bilioni 91zitatumika katika mradi wa maji vijijini na shilingi trilioni 186 zinaingizwa katika mradi wa maendeleo ya umeme vijijini utakaosadia kuleta maendeleo ya viwanda, banki na kuwafanya wananchi ya vijijini kutokimbilia mijini.
Kuhusu hoja ya ongezeko la pensheni kwa wastaafu, Mhe Mkuya amesema serikali baada ya kutafakari imeamua kuongeza kiwango cha fedha kwa wastaafu kutoka shilingi elfu 50 kwa mwezi hadi laki moja badala ya elfu 85 ya awali na kusisitiza lengo la serikali ni kuhakikisha wazee wastaafu wanapata fedha zao kwa wakati ambapo amesema kiwango hicho kitaanza kutumika Julai mosi mwaka huu.
Aidha baadhi ya wabunge wamekuwa na maoni tofauti huku wengine wakionekana kuipongeza kwa madai kuwa inalenga kuondoa umasikini vijijini huku wengine wakisisitiza inalenga kuwaumiza wananchi kwa kuwa imekaa kisiasa kufurahisha wananchi ambapo wamesisitiza umuhimu wa bunge kuwa na kiwango sawa cha idadi ya wabunge ili kuzuia kupitisha mipango isiyo na tija kwa wananchi.
0 maoni:
Post a Comment