Mbunge wa jimbo Songea mjini mkoani Ruvuma Dkt. Emmanuel Nchimbi ametangaza rasmi kutogombea tena ubunge katika jimbo hilo.
Aidha, Nchimbi aliyelitumikia jimbo hilo kwa miaka 10 alikutana na wanachama wa chama cha mapinduzi Katika uwanja wa majimaji mjini Songea pamoja na kuelezea mafanikio mbalimbali ya maendeleo aliyoyafanya katika jimbo hilo ikiwemo ujenzi wa barabara, zahanati na shule za sekondari lakini pia akatumia nafasi hiyo kutangaza rasmi kutogombea tena ubunge katika jimbo la songea mjini.
Kufuatia tamko hilo hali ya simanzi ilizuka kwa baadhi ya wananchi na wanachama wa CCM Songea huku wengine wakiangua kilio.
Wakizungumzia uamuzi huo baadhi ya wananchi katika jimbo hilo wamepingana na uamuzi huo huku wakimuomba mbunge huyo kubadili msimamo wake hata hivyo amesema ameahidi wananchi kwenda kulifikiria suala hilo.
0 maoni:
Post a Comment