MAKAMBA AKUSANYA MAELFU YA WATU MKOANI SHIYNYANGA KAMA LOWASSA

Basi alilopanda Mtangaza nia ya urais Kupitia CCM,January Makamba likiwasili katika ofisi za CCM wilaya ya Shinyanga 
Maelfu ya wakazi wa Shinyanga wakiwa nje ya jengo la Chama Cha Mapinduzi wilaya ya Shinyanga mjini,ambapo leo Naibu waziri wa sayansi na teknolojia nchini January Makamba ambaye ni miongoni mwa watangaza nia kuwania nafasi ya urais katika uchaguzi mkuu ujao 2015 amefika kuchukua wadhamini wake 6,228 wanaomuunga mkono kutoka mkoa wa Shinyanga.

Mheshimiwa January Makamba (Mbunge wa Bumbuli) amepata mapokezi makubwa mkoani Shinyanga,ikiwa ni siku chache tu baada ya mtangaza nia ya urais mwingine mheshimiwa Edward Lowassa kukusanya maelfu ya wakazi wa Shinyanga akisaka wadhamini.

 Waendesha bodaboda wakiendeshs pikipiki kwa mbwembwe wakati msafara wa mheshimiwa January Makamba ukiwasili katika ofisi za CCM wilaya ya Shinyanga mjini
Basi alilopanda Mtangaza nia ya urais Kupitia CCM,January Makamba likiwasili katika ofisi za CCM wilaya ya Shinyanga mjini leo

Wafuasi wa CCM na wakazi wa Shinyanga wakimpokea January Makamba
Mheshimiwa January Makamba akishuka kwenye basi analosafiria kusaka wadhimini katika mikoa mbalimbali nchini
Shangwe,Nderemo na vifijo vikatawala wakati wa mapokezi ya mheshimiwa January Makamba,kijana mwenye umri wa miaka 41 aliyetangaza nia ya kuwania urai nchini Tanzania

Mwalimu Ezra Manjerenga akiwa na walimu wenzake nje ya ofisi za CCM wilaya ya Shinyanga mjini leo ambapo January Makamba amezungumza na wakazi wa Shinyanga na kueleza nia yake ya kuwania urais nchini Tanzania kupitia CCM

Mheshimiwa January Makamba akisalimiana na wakazi wa Shinyanga
Vijana wa sarakasi kutoka Shinyanga wakifanya yao
Mheshimiwa January Makamba akikumbatiana na mmoja wa wadhamini wake mjini Shinyanga

Wadhamini wa mheshimiwa na wakazi wa Shinyanga wakiwa eneo la tukio
Mheshimiwa January Makamba akinong'ona jambo na mbunge wa Shinyanga mjini Mheshimiwa Stephen Masele ambaye ni Naibu waziri ofisi ya makamu wa rais Mazingira 

Shehe wa wilaya ya Shinyanga Sudy Kategire akiomba dua eneo la tukio

Mzee Itendele akiomba eneo la tukio

Mheshimiwa January Makama akiwa eneo la tukio na mke wake Ramona Urassa (First lady mtarajiwa)

 Mbunge wa Shinyanga mjini Mheshimiwa Stephen Masele ambaye ni Naibu waziri ofisi ya makamu wa rais Mazingira akizungumza nje ya ofisi za CCM wilaya ya Shinyanga,ambapo alisema Mheshimiwa January Makamba ana akili timamu na anafaa kuongoza nchi ya Tanzania
Mheshimiwa January Makamba akikumbatiana na mbunge wa Shinyanga mjini Mheshimiwa Stephen Masele ambaye ni Naibu waziri ofisi ya makamu wa rais Mazingira,aliyesimama kushoto ni First Lady mtarajiwa 
Ramona Urassa

Makatibu wa CCM wilaya ya Shinyanga mjini(Charles Sangura) na Magreth Cosmas wa Shinyanga Vijijini wakijiandaa kumkabidhi mtia nia ya urais January Makamba fomu na kadi za wadhamini kutoka mkoa wa Shinyanga

Mtangaza nia ya urais kupitia CCM January Makamba akionesha fomu ya majina ya wadhamini 6,228 kutoka mkoa wa Shinyanga
 
Wakazi wa Shinyanga wakiwa eneo la tukio
Katibu wa CCM wilaya ya Shinyanga vijijini Magreth Cosmas akikabidhi kadi za wadhamini kwa mheshimiwa January Makamba

Tunafutilia kinachoendelea....

 Mkutano unaendelea
Mwalimu Ezra Manjerenga akizungumza eneo la tukio kwa niaba ya walimu wenzake wanaomuunga mkono January Makamba.

Mkurugenzi wa kampuni ya ujenzi Kwilasa Investment,Ndugu Charles Kwilasa akisalimiana na mheshimiwa January Makamba   
January Makamba mwenye umri wa miaka 41,akizungumza ,ambapo amewaomba wajumbe wa kikao cha mkutano mkuu wa CCM utakaopitisha jina la mgombea urais kupitia CCM wapitishe jina lake ili CCM ishinde kwa urahisi zaidi kutokana na kwamba anakubalika na ana ushawishi mkubwa kwa makundi yote katika jamii wakiwemo vijana wenzake.

Mheshimiwa January akizungumza na wakazi wa Shinyanga,ambapo mbali na kuwashukuru kwa kujitokeza kumdhamini pia aliomba upendo,umoja na mshikamano udumu ndani ya CCM.Makamba amesema kuna baadhi ya watangaza nia wanaotumia majukwaa kuwachafua wenzao badala ya kueleza watawafanyia nini watanzania,kitendo alichodai kinaweza kuwagawa wanachama wa CCM.

First Lady mtarajiwa Ramona Urassa (mke wa January Makamba) akiwasalimia wakazi wa Shinyanga

Wakazi wa Shinyanga wakiwa eneo la tukio

Tunafuatilia kinachoendelea hapa...

January Makamba na mke wake Ramona Urassa wakiagana na wakazi wa Shinyanga
Mheshimiwa January Makamba akipanda kwenye basi lake baada ya kukamilisha zoezi la kuona na wadhamini wake na kuzungumza na wakazi wa  Shinyanga.
Picha zote na Kadama Malunde- Malunde1 blog

0 maoni:

Post a Comment