WAZIRI MKUU MSTAAFU SUMAYE ATANGAZA NIA YA KUGOMBEA URAIS

Kasi ya wanachama wa CCM kutangaza nia ya Kugombania Nafasi ya Urais imezidi kuendelea ambapo leo Aliyekuwa waziri mkuu wa awamu ya tatu Mh Fredrick Sumaye ametangaza nia yake ya kuwania nafasi hiyo katika Uchaguzi mkuu wa Mwaka huu.

WAZARI MKUU MSTAAFU SUMAYE


Akitangaza nia yake mbele ya waandishi wa habari na wanachama wa chama cha Mapinduzi katika ukumbi wa Hyatt Regency Kilimanjaro Hotel Sumaye ametaja vipaumbele vyake kuwa ni Kukuza Uchumi,Kuboresha huduma za kijamii pamoja na kupambana na maovu ikiwemo Rushwa,ufisadi na Biashara ya madawa ya kulevya.

Sumaye amesema kuwa amejiandaa kwa dhati kupokea kijiti atakachokiacha Rais wa sasa Mh Jakaya Mrisho Kikwete kwa kuwa amejipima na kuona anajitosheleza kuwatumikia watanzania kwa awamu ya tano ya urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.



Kuhusu kukuza uchumi Mh Sumaye amesema kuwa eneo kubwa linalohitaji msukumo ni kilimo kwa kuboresha mbegu bora na masoko sambamba na kusimamia viwanda vya ndani.

Sambamba na hayo Mh Sumaye amesema kuwa kuhusu kupambana na maovu ataunda chombo na mahakama maalumu ya kushughulikia Rushwa,Ufisadi,Uhujumu uchumi na biashaya ya Madawa ya kulevya.

Akizungumzia sifa za Rais ajaye Sumaye amesema kuwa anatakiwa awe mtu aliye tayari Kujitafakari na kujipima kiakili,Kiafya,kimaadili na kidhamira kwa maendeleo ya Taifa na si ya familia na binafsi.

Mh Fredrick Sumaye amekuwa kiongozi wa saba wa chama cha mapinduzi kutangaza nia ya kugombea nafasi ya urais baada ya Mh Edward Lowassa,Steven Wasirra,Mwigulu Nchemba,Mark Mwandosya na Ally Karume kutangaza nia hiyo.


0 maoni:

Post a Comment