PISTORIOUS HUENDA AKAACHIWA HURU AGOSTI MWAKA HUU

Oscar Pistorious,akilia kwa uchungu
Wakuu wa magereza Nchini Afrika Kuisini wamesema kuwa Oscar Pistorius, ataachiliwa kutoka gerezani mwezi Agosti mwaka huu miezi kumi baadaye, ili atumikie kifungo cha nje, cha hukumu aliyopewa ya miaka mitano.
Bingwa huyo wa nishani ya dhahabu katika mbio za Olimpiki, alikutwa na hatia ya kumpiga risasi bila ya kukusudia na kumuuwa mpenziwe, Reeva Steen-kamp,
na kumuuwa mwana mitindo huyo.
Mahakama kuu Nchini Afrika Kusini mwezi Novemba mwaka huu, itasikiliza rufaa ya waendesha mashtaka ya kujaribu kupunguza makali ya hukumu iliyotolewa dhidi ya mwanariadha huyo mlemavu.

0 maoni:

Post a Comment