KATIBU WA CHAMA CHA WAZALENDO ACT UKEREWE MKOANI MWANZA AZOMEWA MKUTANONI...!!

NA YOHANA EMMANUEL ,UKEREWE

KATIBU  WA  CHAMA  CHA  ACT- WAZALENDO  MKOA WA  MWANZA ROBART  GWANCHELE  AMEJIKUTA  KATIKA WAKATI  MUGUMU BAADA YA  KUZOMEWA  WAKATI  ANAUTUBIA MKUTANO WA  HADHARA MJINI NANSIO WILAYA  YA  UKEREWE JUZI.



SAKATA HILO LILITOKEA MAJIRA  YA SAA 11 JIONI  BAADA YA  KIONGOZI HUYO WA ACT- WAZALENDO    KUDAI KUWA    MBUNGE  NA MADIWANI  WA   [ CHADEMA]  WALIOONGOZA JIMBO  HILO KWA MIAKA MITANO  ILIYOPITA  WAMESHINDWA  KUTATUA  KERO ZA WANANCHI.

AKIZUNGUMZA  HUKU   SAUTI  ZA BAADHI YA  WATU HASA VIJANA  WAKIZOMEA  GWANCHELE  ALISEMA  NYINYI  SI MLICHAGUA  MBUNGE NA  MADIWANI WA CHADEMA 2010?  MBONA  BARABARA AZIPITIKI  NA MNAENDELEA  KUKABILIWA NA  TATIZO LA  MAJI KATIKA    MJINI   NANSIO.

KATIKA  SAKATA  HILO MBALI YA ZOMEA  ZOMEA  PIA  BAADHI  YA  WANANCHI  HUKU BAADHI YAO WAKIONDOKA  WAKIONEKANA  KUKERWA  NA  MADAI HAYO  WALISIKIKA  WAKIMTAKA  ELEZE  SERA ZA CHAMA  CHAKE  NA SIO  KUELEZA   MAMBO AMBAYO UJUI.

NYINYI  SIKILIZENI  TUWAELEZE  UKWELI  VIONGOZI WENU WAMESHINDWA  KUWALETEA MAENDELEO  ALAFU  MNAENDEKEZA   SIASA ZA  USABIKI  NA  KUDAI  KUWA  MBUNGE WA JIMBO HILO SALVATORY MACHEMLI  AMESHINDWA  KUJENGA HOJA BUNGENI  NA KUONDOA  TATIZO LA   USAFIRI  WA  MELI  KATI  YA  UKEREWE NA MJI WA MWANZA.

AKIZUNGUMZA BILA KUTAJA CHAMA  NA MAJINA YAO HUKU HOTUBA YAKE IKIKATISHWA NA ZOMEA ZOMEA  NA MILUZI  ALISEMA   BAADHI YA  VIONGOZI  WA  KISIASA  WANAZUNGUMZA WASICHOTENDA   MFANO  WALIDAI  AWATAPOKEA POSHO  ZA BUNGENI  NA KUTUMIA  MAGARI YA  KIFAHALI LAKINI  HAO HAO NDIO WAKWANZA  KUPOKEA POSHO NA  KUTUMIA  MAGARI  HAYO ALISEMA GWANCHELE.

TUNATAKA MTUUNGE MKONO TUMEKUJA KUWALETEA CHAMA CHA WANYONGE CHA ACT WAZALENDO NA SIO VYAMA VYA WATU AMBAO USIKIKA KATIKA MAJUKWAA WAKIKEMEA MAOVU NA UFISADI WA VYAMA VINGINE WAKATI WAO  NI WAOVU NA  MABEPALI  AMBAO  AWAJUI  SHIDA  ZA WANYONGE ALISEMA  GWANCHELE.


HATA HIVYO ALICHUKUA FUSA HIYO KUWAONYA WANANCHI KUACHA KUSHILIKI MAHANDAMANO YANAYOITISHWA NA VIONGOZI WA KISIASA BILA KUFUATA TARATIBU NA KUONGEZA KUWA MBALI YA VIJANA KUISHIA MAHABUSU NA KUACHA FAMILIA ZAO BILA HUDUMA PIA ALIONGEZA KUWA MAHANDAMANO HAYO  UITISHWA  KUTETEA MASLAI YA  VIONGOZI NA VYAMA  VYAO.

AKIFAFANUA ALISEMA ACT WAZALENDO  AIPINGI  MAHANDANO LAKINI  TUNATAKA  MAHANDAMANO  YA  KUDAI MASLAI  YA  WAKULIMA, WAVUVI NA HATA  WAMACHINGA NA YALIYOANDALIWA KWA   KUFUTA  TARATIBU NA SHERIA.

AWALI AKIFUNGUA MKUTANO HUO MWENYEKITI WA  ACT  WAZALENDO  WA  WILAYA  YA  UKEREWE CHARLES  MUGUNDA PAPAA  AMBAE MBALI YA KUOMBA NA  KUTAAZALISHA YEYOTE  ANAYEKUSUDIA  KUZOMEA AHACHANE NA MAWAZO  HAYO   PIA  ALIDAI KUWA  WAO WAMEKUJA  KUELEZA SERA  ZAO NA SIO  MATUSI NA  KEJERI KWA  VIONGOZI WA VYAMA VINGINE. MWISHO.


0 maoni:

Post a Comment