MSANII RECHO AZUNGUMZIA SKENDO YAKE UA KUTUMIA MADAWA YA KULEVYA..

Msanii wa muziki Recho almaarufu kama Recho Upepo ambaye alitamba na nyimbo kama Upepo, Kizunguzungu, amefunguka na kusema kuwa yeye hatumii madawa ya kulevya kama ambavyo watu mtaani wanavyodai.


"Kiukweli mimi situmii madawa ya kulevya hata kidogo, na huwa naumia sana roho napokuwa naambiwa hizi taarifa juu ya kutumia madawa ya kulevya, siijui hata ladha yake ila nadhani watu wanakuwa wakinifananisha, unajua mimi huwa nafananishwa sana na Ray C hivyo labda ndiyo sababu ya hizi taarifa kuwepo mtanii ila kiukweli mimi si mtumiaji wa madawa ya kulevya" amesema Recho 

0 maoni:

Post a Comment