HANS POPPE NAYE ACHOMA WESE KWENDA KUCHEKI KIKOSI CHAKE...


Simba imeanza Ligi Kuu Bara kwa kuitandika African Sports kwa bao 1-0.



Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe alichukua uamuzi wa kuchoma mafuta kwa kusafiri hadi mjini Tanga.

Lengo la Hans Poppe lilikuwa ni kushuhudia kikosi chake ambacho ameongoza usajili.

Pamoja na kwamba kamati yake ilishirikiana kwa karibu kabisa na kamati ya mashindano na ufundi, lakini ilikuwa lazima Hans Poppe aone kazi aliyoshiriki kwa asilimia kubwa.

"Kweli Hans Poppe alikuwa Mkwakwani kuangalia mambo yalivyokuwa yanakwenda. Inawezekana ameridhika au la, lakini atakuwa ameona na baadaye anaweza kuwa na maoni yake," 

Hata hivyo, mara nyingi, Hans Poppe amekuwa hakosekani mjini Tanga au mikoa mingine Simba inapocheza.

0 maoni:

Post a Comment