Wakati baadhi ya wasanii na wadau mbalimbali wa burudani nchini wakiendelea kuwa na hofu juu ya mfumo mpya unaovitaka vituo vya redio na runinga kuwalipa wasanii mirahaba inayotokana na kucheza kazi zao, serikali imesema imeunda sheria ambayo itavifanya vishindwe kuepuka kucheza nyimbo za wasanii wa ndani.
Akizungumza kwenye uzinduzi wa filamu ya ‘Home Coming’ Mlimani City jijini Dar es Salaam, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Moses Nnauye alisema sheria hiyo inazitaka TV na Redio zenye vipindi vya burudani kuhakikisha 60% ya content ni ya nyumbani.
“Tumeshatangaza kuanzia tarehe moja mwezi wa kwanza 2016 kila muziki wa msanii utakaopigwa kwenye redio ma television utalipiwa.
"Sheria ilishasainiwa na tumekubaliana na watu wa COSOTA wataisimamia na tumeweka kampuni ya kusimamia muziki umepiga mara ngapi na TV gani.
“Mimi nataka watu waniamini historia yangu, waamini watu watalipwa na haki yao wataipata na jasho lao watalipata. Nilichowaambia kila jambo jipya lazima litakuwa na mapungufu ila sheria ndio zitatuongoza, kila redio na TV zenye vipindi vya burudani wanatakiwa kuhakikisha 60% ya content wanayoitoa iwe ya nyumbani, hakuna wakukwepa hili,” alisisitiza Nape.
Pia Nape alisema tayari ameshakaa na wahusika wa nyombo vya habari na kuzungumzia namna ya utekelezaji wa suala hilo.
“Vyombo vya habari ndio wamekuwa wakinisukuma kufanya hivyo, kwahiyo kama wao ndio wameamua hivyo sisi ulikuwa ni utekelezaji na naamini kila kitu kitaenda sawa.”
0 maoni:
Post a Comment