SERIKALI
ya Awamu ya Tano imepongezwa kwa namna ambavyo imetoa kipaumbele katika
Sekta ya elimu chini ya mpango wa elimu bure, na hivyo kuongeza nafasi
na hadhi ya mwanamke katika jamii.
Pongezi
hizo zimetolewa leo na Mke wa Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius
Nyerere, Mama Maria Nyerere wakati wa mahojiano maalum kuhusu
maadhimisho ya miaka 55 ya Uhuru nyumbani kwake Mikocheni Jijini Dar es
Salaam.
“Elimu
imebadili nafasi ya mwanamke katika jamii, tukiangalia wakati tunapata
uhuru wanawake wengi walikuwa bado hawajui kusoma na kuandika,” alisema
Mama Maria Nyerere
Mama
Maria aliongeza kuwa wakati Tanzania ilipopata uhuru mwaka 1961 idadi
ya wanawake walioshika nafasi za uongozi walikuwa wachache sana na
hazikuwa nafasi kubwa jambo ambalo ni knyume na hivi sasa kwani kwa mara
ya kwanza Tanzania ina Makamu wa Rais mwanamama, Mama Samia Suluhu.
Aliongeza
kuwa pamoja na changamoto zilizopo, Serikali za awamu zote zimekuwa
zikijitahidi kuhakikisha zinapiga hatua katika kukabiliana na adui
ujinga.
Kwa
mujibu wa Mama Maria alisema ni faraja kwa Serikali ya Awamu ya Tano
kutambua umuhimu wa watoto kwenda shule kwa kuamua kutoa elimu ya bila
malipo ya Ada, kwani hiyo inasaidia kupunguza watoto wa mitaani.
“Elimu
imeleta ukombozi watoto waliokuwa awaendi shule walikuwa wanajikuta
wanaingia katika makundi ndipo unasikia Panya road, mbwa mwitu na
mengine,” aliongeza Mama Maria.
Aidha
alisema kuwa ili taifa liweze kupata maendeleo ni lazima kujiamini,
kuthubutu na kutenda kama ambavyo sasa Serikali imeamini na kuonesha
uthubutu katika farsafa ya Hapa Kazi Tu na Tanzania ya viwanda.
Mama
Maria ametoa rai kwa wakinamama kushirikiana katika kuhakikisha
wanavitunza viwanda vinavyojengwa ili vieweze kuwa chachu ya maendeleo
ya taifa na jamii kwa ujumla.
0 maoni:
Post a Comment