Waziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo, Nape Nnauye amesema
kuanzia mwakani wizara yake itaanzisha tuzo mahsusi kwaajili ya blog za
Tanzania.
Akizungumza wakati akifunga mkutano mkuu na semina ya wanachama wa
umoja wa waendeshaji wa blog nchini, TBN jijini Dar es Salaam Jumanne
hii, Nape amesema kwa kazi kubwa ambayo blog zimekuwa zikiifanya katika
kuhabarisha umma, ni muda wa kuanza kuwatuza wale wanaofanya vizuri.
Amesema alipata wazo la kuja na tuzo za aina hiyo wakati akisafiri
kwenye ndege na kuona jarida linaloelezea tuzo za blog za Kenya na kuona
kuwa kuna ulazima wa Tanzania pia kuwa na tuzo hizo.
Nape amedai kuwa lengo la tuzo hizo zitakazotolewa mwanzoni mwa mwaka
ujao, zitakuwa ni kwaajili ya kuzisaidia blog kuweza kuwa na
‘specialization’ katika maudhui mbalimbali.
Amesema tayari ameshaanza kuzungumza na makampuni na taasisi
mbalimbali kwaajili ya kudhamini tuzo hizo ili kuhakikisha kuwa washindi
wanapewa zawadi kubwa ili kuwahamasisha zaidi. Ameahidi kuwa tuzo hizo
zitakuwa za kwanza kwa namna zitakazovyoendeshwa kwa uwazi na kwamba
makampuni zaidi yanakaribishwa kuweza kuzidhamini.
0 maoni:
Post a Comment