Maelfu ya watu wamejitokeza kuuaga mwili wa mwanasiasa mkongwe
mwanamke nchini India, Jayalalithaa Jayaram aliyefariki Jumatatu hii.
Jayalalithaa alikuwa ni kiongozi mkuu wa serikali katika jimbo la
Tamil Nadu ambaye alifariki katika hospitali ya Apollo iliyopo mjini
Chennai kwa maradhi ya mswhtuko wa moyo. Kiongozi huyo anatarajiwa
kuzikwa Jumanne hii huku waziri mkuu wa nchi hiyo, Narendra Modi
akitarajiwa kuongoza mazishi hayo.
Jimbo la Tamil Nadu limetangaza siku saba za maombolezi huku serikali
ya mji wa Delhi ikitangaza siku hii kuwa ya mapumziko ya kitaifa
kwaajili ya heshima kwa kiongozi huyo.
Picha: Maelfu wajitokeza kuuaga mwili wa mwanasiasa mkongwe nchini India
Tuesday, December 06, 2016
No Comment
0 maoni:
Post a Comment