Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imeendelea na mpango mkakati wake wa kuhakikisha inatoa elimu ya kodi na inamfikia kila mdau ili kuwajengea uelewa wa masuala ya kodi na uhiyari wa kuilipa.
Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi wa TRA, Diana Masala
Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi wa TRA, Diana Masala
Hivi karibuni mamlaka hiyo ilikutana na wasanii mbalimbali wa maigizo na muziki ili kuwafundisha kuhusu masuala mbalimbali ya kodi pamoja na umuhimu wa kulip
Kaimu Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi wa TRA, Diana Masala, anasema kila msanii mwenye sifa za kulipa kodi anatakiwa kulipa na kwamba huduma nzuri zinazotolewa na Serikali zitatumiwa na kila Mtanzania bila kubagua.
Katika semina na wasanii hao, TRA iliwafundisha kuhusu Kodi ya Mapato pamoja na Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) na kwamba kila mtu mwenye kipato anatakiwa kulipa kodi kwa mujibu wa sheria za nchi.
Sambamba na kuwapa elimu ya kodi, pia ilipokea maoni mbalimbali kutoka kwa wasanii hao ili kuweza kujua changamoto wanazokabiliana nazo waweze kuzitatua ikiwa ni pamoja na kuwatengenezea mazingira mazuri ya kufanya kazi zao zitakazowapatia kipato ambacho watatakiwa kukitumia kulipia kodi.
Pia alisema wasanii wote ambao hawajajisajili wanatakiwa kuhakikisha wanajisajili katika ofisi za TRA kupatiwa Namba ya Utambulisho wa Mlipa Kodi (TIN) na baadaye atakadiriwa kodi anayostahili kulipa kulingana na namna anavyopata mapato yake.
Kila msanii ambaye mauzo ghafi yake hayafikii milioni 20 kwa mwaka atahesabika kama mlipa kodi mdogo ambaye atakadiriwa kodi kulingana na mauzo yake au faida aliyoipata.
0 maoni:
Post a Comment