Vijana wahimizwa kuwa na umoja – Mkutano wa TAMSYA

Katika Mkutano Mkuu wa wadau wa TAMSYA, uliofanyika leo Novemba 12 jijini Dar es Salaam, vijana wa kiislamu wahimizwa kuwa na umoja katika jamii.
Hayo yamebainishwa na wadau mbalimbali akiwemo Rais wa Taasisi hiyo, Ramadhani Ulende ambapo amewataka vijana wa kiislamu kuwa na umoja ili kuimarisha moja ya dhumuni la kuanzishwa kwa Taasisi hiyo.
Pia kiongozi huyo amebainisha kazi mbalimbali wanazofanya ikiwemo kusaidia vijana na wanafunzi nchini kote na kueleza kuwa moja ya malengo ni kutatua changamoto zinazowakabili wanafunzi na vijana kwa ujumla.
Vile vile kiongozi huyo ametoa wito kwa taasisi zingine kujumuika kufanya kazi nao huku akitaja kuwa wao wekuwa wakifanya kazi kwa kuwajengea uwezo vijana kwa kwa kuwapatia mafunzo mbalimbali ya ujasiliamaji na kuwapatia msaada wa kimawazo.
Kwa upande wa Mlezi wa Jumuiya hiyo kwa Mkoa wa Dar Es Salaam, Mzee Issa amesisitiza wanajumuiy hiyo kuwa na undugu, kuwa na mahusiano mazuri yatakayoweza kuwa tija kwa jamii hii ni pamoja na kuhakikisha wanapambana katika kutafuta miradi itakayo weza kutoa ajira.
TAMSYA ni kirefu cha neno Tanzania Muslim Student and Youth Association, ilianzishwa mwaka 1993 na ilifahamika kama TAMSA.
Mnamo mwaka 2010, tarehe 13 mwezi 10 jina la TAMSA lilibadilishwa na kuwa TAMSYA yenye lengo la kuwasaidia vijana na wanafunzi wa kiisalamu katika kutatua changamoto mbalimbali ikiwemo za kimaisha.
Pia TAMSYA imekuwa ikifanya kazi ya kuwapa misaada wanafunzi wenye uhitaji wa kupata elimu ya juu kwa kuwaombea nafasi za masomo au kuwaunganisha na sekta husika pamoja na kuwatengenezea njia.

0 maoni:

Post a Comment