Makala;...KAREKE KARENZI NI NANI...???,MAFAHAMU VILIVYO HAPA

Nchini Rwanda anajulikana zaidi kwa jina fupi KK. Alivyokamatwa ,luteni jenerali Karenzi Karake, mwenye umri wa miaka 54 ni mtu wa kwanza wa ngazi ya juu kutoka kwa orodha ya watu 40 walio na wadhfa mkubwa katika jeshi la RPF orodha iliyotolewa na jaji mmoja wa Uhispania akitaka wakamatwe.
Luteni jenerali Kareke Karenzi

Wanakabiliwa na mashtaka ya madai ya kuhusika katika vitendo vinavotajwa kuwa uhalifu wa kivita uliofanyika dhidi ya wa-Hutu mnamo -1990 huko Kazkazini mwa Rwanda. Miongoni mwa wanaodaiwa kufariki kutokana na matukio hayo ni raia watatu wa ki-Spanish waliokuwa wakifanya kazi ya kutoa misaada ya kibinadamu katika eneo hilo la kazkazini mwa Rwanda.
Jaji muhispania Fernando Merelles ndiye aliyetoa warranti hizo na kutaka wakamatwe,agizo alilolitoa tangu February 2008 .
Serikali ya Rwanda imekuwa ikiighadhabishwa na warranti hizo ikisema hazina msingi wowote. Imekuwa ikishtumu hatua hiyo ya jaji Merelles na kusema ni kutumiwa vibaya na mahasimu wa serikali wenye misimamo mikali na kwamba jaji huyo hajachukua hatua zipasavyo kupata mashahidi kutoka Rwanda au hata kufanya kazi pamoja na mahakama za Rwanda.
Karenzi Karake mwenyewe amekuwa akishikilia nyadhfa mbambali tangu ajiunge na RPF hapo 1980 baada ya kufanya kazi na jeshi la nchi jirani , Uganda National Resistance Army. Kisha akawa kama afisa wa kiungo cha kati cha RPF huko Kigali wakati wa mazungumzo ya kutafuta amani ya Rwanda baina yao na iliyokuwa serikali ya wa- Hutu nchini humo wakati huo.
Mkataba huo wa amani ulitiwa saini mwezi wa nane tarehe 4, 1993. Baada ya mauaji ya kimbari ya 1994 na RPF ilipochukua madaraka , KK alipewa vyeo mbalimbali katika jeshi la nchi hiyo ikiwemo kuwa mkuu wa kitengo cha intelijensia , mafunzo na oparesheni mbalimbali. Alipokuwa kamanda wa kikosi cha Rwanda aliongoza kikosi chake katika vita baina ya Rwanda na Congo hapo mwaka 2000.
Kati ya mwaka 2007-09 alikuwa naibu kamanda wa kikosi cha pamoja cha walinda amani cha Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika huko Darfur. Imeripotiwa kuwa Umoja wa mataifa ulishinikizwa kutoendeleza mkataba wake baada ya makundi ya kutetea haki za binadamu kuelezea wasiwasi wao kuhusu yeye kuendelea na wadhfa huo huku warranti hizo zikiwa zimeshatolewa huko Uhispani.
Ikabidi cheo hicho apewe afisa mwengine ambao hakuwa kwenye orodha hiyo ya watuhumiwa.
Luteni jenerali Karenzi Karake amekuwa mkurugenzi mkuu wa taasisi hiyo ya intelligensia na huduma za usalama nchini Rwanda na amesifiwa sana na serikali ya nchi hiyo kama shujaa katika ngazi za RPF aliyepambana kusitisha mauaji ya kimbari dhidi ya wa Tutsi.

0 maoni:

Post a Comment