Kitabu cha rekodi cha Guinness kinatambua hizi Rekodi mbili kubwa duniani alizoweka Sam Smith na muziki wake.

sam-smith-billboard-650_0
Mwimbaji Sam Smith anatambulika na kitabu cha rekodi ha Guinness World Records kwa rekodi mbili mpya alizoweka hivi karibuni.
Msanii huyu kutoka Uingereza aliyeimba wimbo unaotumika kwenye filamu mpya ya James Bond   Spectre ‘Writing’s on the Wall’ umekuwa wimbo wa kwanza ndani ya miaka 50 ya filamu hizi kushika namba moja kwenye chati za Uingereza za nyimbo.
Rekodi ya pili aliyoweka ni ya album yake ya kwanza  “In The Lonely Hour” iliyoshika namba moja kwenye chati za album za Uingereza kwa wiki 69 kwa mfululizo bila kushuka.
Sam Smith amevunja rekodi ya Emeli Sande,ambaye album yake ya “Our Version of Events” ilika wiki 63.

0 maoni:

Post a Comment