Serikali yakaribisha viwanda kutoka China

Waziri mkuu, Kassim Majaliwa amesema kuwa serikali ya Tanzania itaendeleza ushirikiano wake na nchi ya China, katika nyanja mbalimbali ikiwemo sekta ya viwanda, nishati na miundombinu kupitia uwekezaji.
Waziri Majaliwa ametoa kauli hiyo Jumatatu hii jijini Dar es Salaam, wakati wa mazungumzo yake na waziri wa mambo ya nje wa China, Wang Yi kwa niaba ya Rais Dkt John Magufuli ambapo amesema Tanzania ipo tayari kupokea makampuni kutoka China kuja kuwekeza katika maeneo mbalimbali nchini.
“Tanzania iko tayari kupokea kampuni zaidi za China kuja kuwekeza katika maeneo mbalimbali nchini.Tupo tayari kupokea viwanda kati ya katika kipindi cha miaka mitatu ijayo,” amesema.
Kwa upande wake, Wang amepongeza utendaji kazi wa Rais Magufuli pamoja na viongozi wengine hususan katika mapambano dhidi ya rushwa na ufisadi na tayari matunda yameanza kuonekana.
“Serikali ya China kwa sasa iko katika mkakati wa kuhamishia viwanda vyake vingi barani Afrika. Iliamua kuichagua Tanzania kuwa moja katika ya nchi watakayohamishia viwanda hivyo kutokana na kuridhishwa na dhamira inayoonyeshwa na serikali katika kuleta maendeleo,” alisema Wang.
Waziri Wang, yupo nchini kikazi kwa ziara ya siku moja ya kikazi hivyo anatarajiwa kuondoka hii leo.

0 maoni:

Post a Comment