Baadhi ya wabunge wameitaka serikali kupambana na vyanzo vikubwa vya uhakika vya kodi ikiwemo makampuni ya simu za mkononi badala ya kuongeza kodi kwenye mafuta na kusababisha wananchi kuishi katika mazingira magumu.

Wakichangia mswada wa sheria ya fedha wa mwaka 2015, baadhi ya wabunge wamehoji uwezo wa serikali wa kuyakabili makampuni makubwa ili yaweze kulipa kodi hususani katika mfumo wa soko huria ambapo baadhi ya makampni yamekuwa na mapato makubwa kuliko ya serikali.
 
Awali akiwasilisha maoni ya kamati ya kudumu ya bunge ya bajeti, Mheshimiwa Josephat Kandege amesema kutokana na kutokuwa na tafsiri sahihi ya mafuta ghafi serikali imekuwa ikikosa mapato stahiki na kuitaka kufanya uchunguzi, huku msemaji wa kambi ya upinzani Mhe.Joseph Mbatia akiendelea kusisitiza kuwa kuongeza kodi katika mafuta kutawaumiza wananchi.
 
Aidha akiwasilisha mswada wa sheria ya fedha hususani matumizi ya sukari inayotumika viwandani, waziri wa fedha na uchumi Mhe Saada Mkuya Salum amesema serikal imepunguza kodi hadi asilimia 25 kutoka asilimia 50 ya awali kwa waagizaji wa sukari ili kutoathiri mitaji ya wafanyabiashara.
Wakati Tanzania ikitarajia kufanya uchaguzi mkuu hapo Mwezi Oktoba mwaka huu,wanasiasa mbalimbali wameanza kujitokeza katika vyama vya siasa hapa nchini  kuomba ridhaa ya  vyama vyao katika kupeperusha bendera za vyama hivyo katika uchaguzi huo.  
     

Hapa wilayani Tarime mkoani Mara Mbunge wa Viti Maalum kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Bi Esther Matiko amejitosa rasmi kuomba ridhaa ya Chama hicho kupeperusha Bendera ya CHADEMA katika kugombea nafasi ubunge wa jimbo la Tarime.

Katika kuhakikisha wananchi wa wilaya hiyo wanapiga kura kwa ukamilifu katika uchaguzi mkuu hapo mwezi oktoba mwaka huu,Bi Esther Matiko ametoa rai kwa wananchi wilayani humo kujiandikisha katika daftari la wapiga kura.

Mapema kabla ya mkutano wa hadhara,Bi Esther Matiko alipata mapokezi kutika eneo la Mika na kIsha kuchukua fomu ya kuomba ridhaa ndani ya chama hicho cha hicho katika ofisi za  CHADEMA.
Bunge limesikia maoni ya wadau ya kuuondoa Bungeni Muswada wa Sheria ya Haki ya Kupata Habari 2015 ambao ulitarajiwa kusomwa kwa mara ya pili Juni 27, mwaka huu.
Katibu wa Bunge, Dk. Thomas Kashililah, alithibitisha hayo jana kwenye viwanja vya Bunge wakati akihojiwa kutaka kujua iwapo ushauri wa kamati umemfikia Spika na uamuzi juu ya suala hilo.
“Ushauri wa kamati umezingatiwa, Muswada umeondolewa Bungeni,” Dk. Kashilillah.
Aidha, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju, alisisitiza kuwa maoni ya wadau hayawezi kupuuzwa katika uandaaji wa Muswada wa Sheria ya Haki ya Kupata Habari, 2015.
“Hatutapuuza maoni ya wadau hasa yanayolenga kuboresha muswada husika. Utungaji wa sheria yoyote ni lazima uwe shirikishi, hivyo maoni ya wadau yamesikikizwa kama ilivyokuwa awali walishauri Muswada huo na ule wa Huduma kwa Vyombo vya Habari, usije kwa hati ya dharura, tulizingatia na uliondolewa,”alibainisha.
Juni 22, mwaka huu, wadau mbalimbali wa habari waliokutana jijini Dar es Salaam, walipinga miswada hiyo kwa kile kinachoelezwa kuwa inakiuka sheria za kimataifa, Katiba ya nchi na kuwanyima haki raia kupata taarifa na kuua ndoto ya vijana wanaotarajia kunufaika na tasnia ya habari.
Wadau hao ni Chama cha Wamiliki wa Vyombo vya Habari Tanzania ( MOAT), Baraza la Habari Tanzania (MCT), Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA) Tawi la Tanzania na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu ( THRDC).
Mmiliki wa Kampuni ya New Habari Corperation, Rostam Aziz, alisema muswada huo ni mbaya kwani unazuia dhana nzima ya uwazi na ukweli hivyo kulirudisha taifa nyuma na kuitaka serikali kutopeleka bungeni hadi wadau wote wa tasnia ya habari watakapotoa maoni.
“Serikali isifanye haraka, muswada huu utaturudisha nyuma kama taifa. Usitishwe kupelekwa bungeni hadi pale wadau wote watakapotoa maoni yao,” Rostam.
Katibu Mtendaji wa MCT, Kajubi Mukajanga, alisema baraza hilo limetoa ombi hilo kwa sababu wadau wa habari hawakuwa na muda wa kutosha kutoa maoni yao baada ya kusomwa kwa mara ya kwanza wiki iliyopita.


Siku chache zimepita tangu Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ kushinda kesi na kumchukua mtoto wake Sasha, aliyezaa na mwanadada Faiza Ally, kwa madai kuwa mzazi mwenzake huyo ameshindwa kumlea kutokana na kukosa maadili,  hatua hiyo imepelekea Faiza kukata rufaa ya kutaka arudishiwe mtoto wake.
 
Kupitia mtandao wa kijamii amesema kuwa “Nasitikishwa sana na maneno yenu makali hasa nyinyi mnao sambaza kashfa juu yangu kuhusu mavazi yangu- hakuna hiyo sheria tanzania inayosema nipokonywe mtoto kuhusu mavazi yangu”.
 
“Nimekata rufaa na nawahakikishia nitashinda kesi na nitamlea mwanangu na nitavaa mavazi yangu na nita enjoy maisha yangu/ nina mwanasheria makini aliesomea sheria na sisi nyinyi mnao nipa hukumu humu ndani na kwingine! pamoja na mavazi yangu mimi ni mama bora!”
 
“Mnajua upande wangu lkn hamjui upande wa sugu na hakika mengi mtayajua kupitia kesi hii/ mavazi yangu nayapenda na kwa mujibu wa sheria si kitu kinacho nifanye ni pokonye mtoto wangu-maneno yenu machafu dhidi yangu yananiuma sana lakini kamwe hayata nirudisha nyuma katika kutetea haki yangu!”.
 
“Namjua sugu na na ninajiua mm ktk ubora wangu katika malezi ya mwanangu/ mm ni mama na si mama tu ni mama bora kwa sasha na ananihitaji na sitamuacha na nyinyi wajinga wachache endeleeni kuniponda na kuona na stahili kupata pigo hili na si wote”.
 
“Kuna wengine wema kwa upande wangu na washukuru na nina waahidi sitawarudisha nyuma nitasimama mpaka kieleweke
WAKULIMA wa zao la Mpunga kwenye bonde la Usangu Wilaya ya Mbarali Mkoani Mbeya wamesema matumizi ya mbegu za mpunga zisizo na ubora zinachangia kwa kiasi kikubwa  kupata mavuno yasio na tija na kushuka kwa soko  huku wakilalamikia ujazo la rumbesa kwa gunia.
 
Wamesema haya wakati wa siku ya Mkulima, iliyoandaliwa na Kampuni ya Mtenda Rice Supply inayojishughulisha na masuala ya Kilimo Mkoani Mbeya ambapo wanasema ikiwa watapata elimu ya kutosha  juu ya mbegu bora za mpunga kilimo chao kitakuwa na tija.
 
Aidha Mkurugenzi wa Kampuni ya Mtenda Rice Supply, George Mtenda amewataka wakulima kuorodhesha majina yao mapema Septemba mwaka huu ili waweze kupata elimu ya matumizi ya mbegu bora na kilimo cha kitaalamu, pamoja na kukopeshwa pembejeo za kilimo.
 
Hata hivyo katika bonde hili vijana wengi wanajihusisha na kilimo cha mpunga ambapo wameshauri vijana wengine kujikita kwenye kilimo na kuacha tabia ya kukimbilia mijini.
Kocha mpya wa Taifa Stars, Charles Boniface Mkwasa aliyechukua nafasi ya Mart Nooij ametangaza kikosi chake kipya kwa ajili ya kuivaa Uganda huku akimtema kipa Deogratius Munish ‘Dida’ na nafasi yake amemchagua Ally Mustapha ‘Barthez’.

Wengine ambao Mkwasa amewatema ni Erasto Nyoni, Amri Kiemba na Kelvin Friday kutoka Azam FC pia Oscar Joshua kutoka Yanga, Pia Ibrahim Ajibu kutoka Simba.


Waliorejea ni Kelvin Yondani pia Deus Kaseke huku akimchukua Michael Idan wa Ruvu Shooting.
Pia Samuel Kamuntu wa JKT, Juma Abdul wa Yanga na Mudathir Yahya kutoka Azam wamejumuishwa kwamba wanaweza kuitwa wakati wowote.

KIKOSI KAMILI:
Mwadini Ally-Azam
Ally Mustapha-Yanga
Mudathir Khamis-KMKM
Shomari Kapombe-Azam
Michael Haidan-Ruvu Shooting
Mohammed Hussein-Simba
Mwinyi Hajj-KMKM
Nadir Haroub-Yanga
Kelvin Yondani-Yanga
Aggrey Morris-Azam
Hassan Isihaka-Simba
Jonas Mkude-Simba
Abdi Banda-Simba
Simon Msuva-Yanga
Said Ndemla-Simba
Ramadhan Singano-Simba
Salum Telela-Yanga
Frank Domayo-Azam
Atupele Green-Kagera Sugar
Rashid Mandawa-Mwadui
Ame Ally-Azam
Deus Kaseke-Yanga
Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wanadaiwa kumzuia Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad  kuhudhuria shughuli ya kuvunjwa kwa Baraza hilo inayotarajiwa kuongozwa na Rais wa Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein kesho, kufuatia kitendo cha Mawaziri na Wawakilishi wa CUF kususia kupitisha bajeti kuu ya Serikali ya mwaka wa fedha 2015/16.
 
Azimio hilo limetolewa na wajumbe wa Chama cha Mapinduzi, baada ya Spika wa baraza la wawakilishi Pandu Ameir Kificho kuwataka wajumbe wa baraza hilo kutengua kanuni ili kuruhusu viongozi wa kitaifa akiwemo Rais wa Zanzibar, Makamu wa Kwanza wa Rais na Jaji Mkuu waruhusiwe kuingia ndani ya ukumbi wa baraza wakiwa kama wageni waalikwa.
 
Wakizungumza mara baada ya azimio hilo kupitishwa, Kaimu Mnadhimu wa Baraza hilo wa CCM, Ali Salum Haji, Mwakilishi wa viti maalum Asha Bakari na Mwakilishi wa jimbo la Raha Leo Nassor Salum Aljazeera wamesema hakuna sababu ya kumruhusu Maalim Seif kuhudhuria shughuli hiyo wakati Mawaziri na Wawakilishi wanaotokana na chama chake cha CUF wakiwa wamegoma kuhudhuria shughuli za baraza hilo.
 
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Mambo ya Nje na Mwakilishi wa jimbo la Mji Mkongwe wa CUF, Ismail Jussa Ladhu amesema tayari chama chake kimeanza kuchukua hatua kwa kuziandikia barua taasisi zenye dhamana na mambo ya uchaguzi, vyombo vya dola na jumuiya za kimataifa kuhusu ukiukwaji wa taratibu za uchaguzi unavyofanyika Zanzibar na dhamira ya wajumbe wa CCM ya kutaka kuvunja Serikali ya Umoja wa Kitaifa.

SIKU moja baada ya tukio la wauguzi wawili wa zahanati iliyopo Kijiji cha Shishiyu, Wilaya ya Maswa, mkoani Simiyu kudaiwa kumfukuza mama mjamzito aliyejifungulia bafuni katika nyumba iliyopo jirani na zahanati hiyo, uongozi wa halmashauri hiyo umewahamisha kituo cha kazi wauguzi hao badala ya kuwachukulia hatua.

Wauguzi hao (majina yanahifadhiwa), wanadaiwa kumfukuza mama aliyekuwa mjamzito Rotha Bujiku baada ya kufika katika zahanati hiyo ili aweze kupatiwa huduma ya kujifungua.

Akizungumza na waandishi wa habari juu ya hatua ambazo zimechukuliwa kwa wauguzi hao, Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Trasiasi Kagenzi, alisema wauguzi hao wamehamishwa kituo cha kazi na kupelekwa katika kituo kingine.

Alisema uongozi wa halmashauri umeona kabla ya kuwachukulia hatua za kinidhamu, uwahamishe kituo ili kuokoa maisha yao kwa kuwa wakazi wa kijiji hicho walikuwa wanataka kuwadhuru.

Aliongeza kuwa, hawakuona haja ya kuanza kuwachukulia hatua za kisheria wakati maisha yao yapo hatarini hivyo wamewanusuru kwanza na baadaye watachukuliwa hatua za kinidhamu.

"Suala la kuwahamisha na kuwachukulia hatua za kinidhamu ni vitu viwili tofauti...tukumbuke kuwa, kumchukulia mtumishi wa umma hatua za kinidhamu kuna taratibu zake.

"Kutokana na hali hiyo, tumeona hatua ya awali ni kuwatoa katika zahanati hii kwa sababu wananchi walitaka kuwadhuru kwa kitendo walichokifanya," alisema Kagenzi.

Alisema uongozi ulikaa na kutafakari kwa kina wakaona kuna haja ya kunusuru maisha ya wauguzi hao wakati utaratibu wa
kuwachukulia hatua za kinidhamu ukiendelea na kuwahamisha kituo cha kazi hakizuii wasichukuliwe hatua.

Kagenzi alisema watumishi hao watachukuliwa hatua za kisheria baada ya uchunguzi kufanyika na kusisitiza kuwa, afya ya mama huyo na mtoto wake zinaendelea vizuri, huduma katika zanahati
hiyo pia zinaendelea baada ya kupelekwa wauguzi wengine.

Aliongeza kuwa, wauguzi hao wamepelekwa katika vituo viwili tofauti ambapo mmoja kapelekwa Kituo cha Mwasayi kilichopo Kata ya Masanmwa, mwingine kapelekwa Zahanati ya Magereza Malya iliyopo Kata ya Buzinza na Mganga Mfawidhi amepelekwa Zahanati ya Bugalama ambazo zote zipo wilayani humo.

Wauguzi hao walifanya tukio hilo juzi kwa kile kilichodaiwa mama huyo walishampa maelezo ya kwenda kujifungulia katika Hospitali ya Wilaya hiyo kutokana na kujifungua mfululizo ambapo alikuwa amekwenda kujifungua mtoto wa 11.


Click image for larger version. 

Name: kamukara.jpg 
Views: 0 
Size: 23.9 KB 
ID: 263445
Edson Kamukara enzi za uhai wake


Ofisa uhusiano wa NMB,Viccent Mnyanyika akimkabidhi zawadi marehemu Edson Kamukara wakati wa uhai wake kwenye utoaji wa tuzo za umahiri wa uandishi wa habari tanzania(EJAT)zilizofanyika Aprili 24 mwaka huu katika ukumbi wa Mlimani city jijini Dar es Salaam,ambapo marehemu alikuwa mshindi wa tatu,anayefuata kutoka kushoto ni Victor Bariety(mshindi wa pili),akifuatiwa na mshindi wa pili.
Taarifa zilizokifikia chumba cha habari zinaarifu kuwa Mwandishi wa habari Edson Kamukara aliyewahi kuandikia gazeti la Tanzania Daima na baadae kuhamia Mwanahalisi, amefikwa na umauti leo jioni baada ya kulipukiwa na jiko la gesi nyumbani kwake Mabibo jijini Dar es Salaam.

Aidha habari kutoka kwa majirani zinaarifu kuwa Kamukara amerejea kutoka Bukoba, na alijisikia vibaya wakati anaenda dukani kununua dawa akaanguka na majirani kusaidia kumpepea na baade kupelekwa kwake ambako alipumzika hadi alipopata nguvu na kuamua kujiandalia chakula na ndipo ajali hiyo kumfika na kugharimu maisha yake.

Mwandishi nguli wa habari,Dotto Bulendu,katika ukurasa wake wa Facebook ameandika haya:

NAKULILIA EDSON KAMUKARA
Ulinikuta Chuo Kikuu nikiwa mwaka wa tatu,ghafla ukawa rafiki yangu wa karibu,ulipenda sana vipindi vyangu nilivyokuwa naendesha pale kwenye kituo cha redio cha chuo kikuu cha Mtakatifu Augustino(Mwanza)(RADIO SAUT),nikiwa mwanafunzi nilikuwa naendesha kipindi cha majadiliano kinachoitwa MTAZAMO MKALI,uliniomba kuja kutazama navyokifanya.

Ulikuja kama mtazamaji mara tatu,baadae nikakuachia uwe unakiendesha,ukawa mahiri sana,nilipomaliza Chuo,niliajiriwa hapo Chuo Kikuu kama mkurugenzi wa kituo cha redio cha chuo kikuu,ili kuifanya redio ishindane,niliimua kutengeneza timu ya kunisaidia,EDSON KAMUKARA ulikuwa chaguo langu.

Nikakuomba ukubali kuwa meneja wa vipindi na kuwa msaidizi wangu mkuu,ulifanya kazi hiyo mpaka ulipomaliza masomo yako ya Chuo Kikuu,ulijiunga na gazeti la majira.

Kabla hujaacha kazi gazeti la majira na kwenda Jambo leo,uliniomba ushauri,na hata ulipoamua kuondoka Jambo leo uliniomba ushauri,nakumbuka wakati unaondoka gazeti la Jambo leo,ulinipigia simu saa sita usiku na kuniambia,"Brother naondoka jambo leo".

Ukanieleza kinagaubaga sababu za kuacha kazi Jambo leo,nami nikakuambia tafuta maisha zaidi ya hayo,ukaondoka na kwenda Tanzania Daima.

Kuwepo kwako Tanzania Daima,kulinifanya nami kuwa mwanafamilia wa Tanzania daima,ni wewe uliyenikutanisha na wafanyakazi wa Tanzania daima,kila nilipokuja Dsm,ilikuwa lazima nije Tanzania daima kuwasalimia.

Nilipoanza kazi Star TV,nilikushirikisha,ukanipa mawazo,umekuwa mshauri wangu,kila napomaliza kipindi ulikuwa unanipa feedback.

EDSON KAMUKARA,mara ya mwisho tulikaa meza moja Mlimani City tulipokwenda kupewa tuzo za umahiri wa habari,leo umekwenda,nakumbuka kabla hujaacha kazi Tanzania Daima na kwenda Mawio ulinipigia simu usiku,nikakwambia,"Oooooooh,unakwenda kumjoin Kubenea?".

Tukacheka sana,leo asubuhi nikakupigia simu,tukaongea kuhusu makala yako ya leo,tukacheka sana,leo jioni naambiwa umefariki dunia,Ooooh,EDSON KAMUKARA,umekwenda wapi mdogo wangu,nani atanipa feedback kila napomaliza kipindi EDSON?

Kweli umekwenda EDSON?nakulilia ,EDSON,Kila majadala wa kipindi cha jicho letu unapokuwa mgumu nilikuwa namuambia Mzee mpendu muite Kamukara na Balile hapa ndiyo mahali pao,sasa umetuacha,EDSON.

If possible amka my young brother,tulikupenda ila Mungu kakupenda zaidi,Tangulia Edson,ndugu,jamaa na rafiki zako tunakulilia,Ahsante Mungu kwa zawadi ya Edson,ulimleta na sasa umemchukua,Tangulia EDSON KAMUKARA.


Wananchi wa wilaya ya Masasi mkoani Mtwara wamelazimika kuzima moto katika soko kuu la mji wa Masasi kwa saa nane kwa kutumia mchanga na maji baada ya kukosekana kwa gari la zimamoto. 

Soko hilo linawafanyabiashara zaidi ya elfu mbili na linategemewa na wilaya za Nanyumbu na Nachingwea, wakizungumza kwa masikitiko baadhi ya waathirika wamesema moto huo ulizuka majira ya saa nne usiku, na serikali haikuweza kusaidia lolote na hapa wanafafanua. 

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Masasi Bernad Luta ambaye alitembelea soko hilo ameiagiza kamati ya maafa ya wilaya kufanya tathimini haraka ili kubaini hasara iliyopatikana, huku akikiri wilaya hiyo kwa sasa haina gari la zimamoto. 

Mbali na viongozi wa serikali waliotembelea soko hilo pia viongozi wa kisiasa kikiwemo chama cha mapinduzi, Chadema na mwenyekiti wa ACT Zitto Zuberi Kabwe ambaye yuko wilayani Masasi amewatembelea wafanyabishara na kuwapa pole.

mipiraa

Wanafunzi katika shule ya Isaac Newton Academy iliyoko Ilford, Uingereza wamezindua mipira ya kiume ‘kondomu’ yenye uwezo wa kugundua maradhi ya zinaa wakati watumiaji wanapokutana kimwili.
Kondomu hiyo inayojulikana kama S.T.EYE inabadili rangi pindi inapokutana na majimaji ya mtu anayeugua maradhi ya zinaa.

mipira

Kulingana na wanafunzi hao kondomu hiyo inabadili rangi tofauti kulingana na bakteria waliopo kwa muhusika.
Kutukana na kuvumbua mipira hiyo wanafunzi hao tayari wametunukiwa tuzo ya ubunifu na kampuni ya ubunifu wa kiteknolojia ya ‘the TeenTech’ pamoja na pauni 1,000.
Wanafunzi hao wamesema wameamua kufanya hivyo kwa lengo la kusaidia vizazi vijavyo ili kuepukana na maradhi yanayoweza kuzuilika kitaalam.


Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya Arumeru na Diwani wa kata ya Mlangarini wilayani humo, Mathias Manga, amenusurika kuuawa baada ya watu wasiojulikana waliokuwa wakimfuatilia kumpiga risasi nje ya geti la nyumba yake. 

Tukio hilo lilitokea saa 4:45 usiku wa kuamkia jana. 

Manga ambaye pia ni mfanyabiashara maarufu wa Tanzanite huko Mirerani, mkoani Arusha ni mmoja kati ya marafiki wakubwa wa Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, ambaye ametangaza nia ya kuomba ridhaa ya CCM kumteua kuwa mgombea wa kiti cha urais katika uchaguzi mkuu mwaka huu. 

Manga alikuwa Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya kumtafutia wadhamini Lowassa mkoani Arusha, kazi ambayo ilikamilika jana baada ya kupata wadhamini 12o,339. 

Haijafahamika rasmi iwapo tukio la kupigwa risasi na kujeruhiwa kwake, lina uhusiano wowote wa kibiashara au kisiasa, kwa sababu Manga mwenyewe hakutaka kuzungumza na waandishi wa habari kuhusiana na suala hilo. 

Hata hivyo, akizungumza kwa njia ya simu na waandishi wa habari jana, Manga alithibitisha kutokea kwa tukio hilo. 

Awali alisema angezungumza na waandishi wa habari baada ya nusu saa kwa vile alikuwa katika mazingira ambayo hayakuwa mazuri kuzungumza, lakini alipopigiwa tena simu alisema hawezi kuzungumza chochote. 

Akizungumza kwa njia ya simu jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo eneo la Ngarenaro. 

Alisema risasi hiyo ilimparaza Manga maeneo ya ubavu wa kulia. 

“Alitoka katika shughuli zake za kawaida na alipokuwa anarejea nyumbani kwake eneo la Ngarenaro kwenye nyumba za Shirika la Nyumba la Taifa, ghafla aliona gari likimfuata kwa nyuma na alipokuwa akitembea kwa kasi nalo liliongeza mwendo, akahisi watu hao wanamfuata, hivyo akazidi kuongeza mwendo hadi alipofika getini kwake na lile gari pia lilieggeshwa kwa nyuma yake," alisema. 

Alifafanua kuwa baada ya kuegesha gari hilo, kati ya wale mmoja wao alishuka akiwa ameshika kisu na mwingine bunduki. 

Kamanda Sabas aliongeza kuwa baada ya Manga kuona hivyo, naye alitoa bastola yake kwa lengo la kujihami. 

"Manga alipotoa silaha yake ili kujilinda, alishtukia akipigwa risasi lakini kwa bahati nzuri haikumpata vizuri…ilimpata maeneo ya nyama kwenye mbavu upande wa kulia na watu hao wakakimbia.” 

Alisema kwa maelezo ya Manga watu hao walikuwa watano na wote walikimbia bila kuchukua kitu chochote na yeye alipelekwa Hospitali ya Mkoa wa Arusha ya Mount Meru kwa matibabu ambako alipata matibabu na kuruhusiwa kurudi nyumbani kutokana na kutoumia sana. 

Kamanda Sabas aliongeza kuwa Jeshi la Polisi linawatafuta wahusika wa tukio hilo kwa njia zote ili wakipatikana wachukuliwe hatua za kisheria. 

LOWASSA ASIKITIKA ATOA POLE 
Lowassa jana wakati wa kudhaminiwa mkoani Arusha jana, alimpa pole Manga kutokana na tukio hilo kinalidaiwa kufanywa na majambazi. 

Lowassa alisema anashukuru Mungu kwa kumnusuru na kusema kwamba anamtakia afya njema ili aendelee na kazi zake. 

ASEMA HATISHWI 
Wakati huo huo, Lowassa amesema hatishwi na vitendo vya kejeli, matusi yanayotolewa dhidi yake na havitamkatisha tamaa katika safari yake ya matumaini na kusisitiza anatosha kuwa Rais. 

Lowassa aliwasili jana jiji hapa akitokea Dodoma. 

Baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa ya Kilimanjaro (KIA), alianza safari yake kwa magari kuelekea Arusha kusaka wadhamini. 

Akiwa njiani msafara wake ulizuiwa na wananchi mara zaidi ya mara tatu wakati akielekea katika Chuo cha Biblia cha Sakila cha kanisa la International Evangelism Church wilayani Arumeru ambapo alialikwa kwaajili ya kuombewa. 

Akitoa neno la shukurani katika kanisa hilo, Lowassa alisema waendelee kupiga magoti na kumuombea ili aweze kufanikiwa katika safari yake ya matumaini kwani safari hiyo ina milima na mabonde. 

Alisema kumekuwapo na maneno ya kejeli yanayotolewa dhidi yake na matusi lakini hata kata tamaa kwani yeye binafsi anaona anafaa kuwa Rais kuwatumikia watanzania. 

“Nipo katika harakati za kutafuta wadhamini ambao hawapatikani kanisani wanapatikana mtaani ambako ndiko CCM ilipo, la kwanza naomba mniombee nayaweza yote kwa yeye anitiae nguvu, naomba mpige magoti msali sana,” alisema Lowassa. 

Akizungumza katika Ibada ya maombezi, Askofu wa kanisa hilo, Dk. Eliudi Isanja, alisema anajua Lowassa anagombea urais na wanamuombea katika safari yake ambayo anaamini watanzania wengi wanaungana nayo. 

Awali katika neno lake la shukurani alianza kwa kumpa pole Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM (NEC) wilaya ya Arumeru Mathias Manga, ambaye alivamiwa na majambazi wakampiga risasi lakini anashukuru hali yake inaendelea vizuri. 

“Mungu ni mwema sana lakini kwa bahati nzuri haijaingia mwilini, tunaendelee kumuombea Afya yake iendelee vizuri ili afanye shughuli zake kwa amani,” alisema Lowassa. 

Akitangaza waliojitokeza kumdhamini Katika Mkoa wa Arusha,Katibu Mwenezi wa CCM Mkoani humo, Issac Joseph, alisema Lowassa amedhaminiwa na wanachama wa CCM 120,336 kati ya wanachama hai 198,795. 

Akiwashukuru wanachama waliojitokeza kumdhamini, Lowassa alisema anawashukuru waliomdhamini na imani yao kwake ataijibu kwa vitendo. 

Alisema haiendi Ikulu kung’aa macho bali anaenda kuhakikisha kupambana na umasikini na atafanya maamuzi magumu kuhakikisha aleta ajira kwa wingi nchini na viwanda kwa wingi ili ajira zapatikane na watu waondokane na umaskini. 


Edward Lowasa ameendelea kuvunja rekodi ya idadi ya watu wanaojitokeza kumdhamnini baada ya kupata wadhamini 120,392 jana  mkoani  Arusha.
 
Rekodi hiyo ya Arusha imezipiku ile iliyowekwa na mkoa ya Iringa alikodhaminiwa na wanachama 58,562.
 
Mbunge huyo wa Monduli aliwasili jijini Arusha saa 9:00 alasiri na kupokelewa kwa mbwembwe zilizoambatana na nyimbo mbalimbali za wasanii kadhaa nchini. Lowassa aliongozana na mkewe Regina na viongozi kadhaa wa CCM.
Mara baada ya kuwasili uwanjani hapo, Lowassa alifanyiwa maombi rasmi na wazee wa kimila wa jamii ya Wamaasai, maarufu kama Malwaigwana.
 
Katibu mwenezi wa CCM mkoa wa Arusha, Isaack Joseph alisema waliomdhamini waziri huyo mkuu wa zamani ni wanachama hai kutoka wilaya zote saba za kichama mkoani Arusha.
 
Kwa CCM, mkoa wa Arusha una wilaya za Arusha Mjini, Karatu, Longido, Monduli, Ngorongoro, Arumeru Mashariki na Arumeru Magharibi.





Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akilakiwa na Kikundi cha Ulinzi wa Jadi cha Sungusungu, alipowasili katika Kijiji cha Hungumalwa njaia panda ya Mwamashinga alipoanza ziara Jimbo la Kwimba, mkoani Mwanza, ya kuimarisha uhai wa chama, kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi pamoja na kusikiliza kero za Wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.




Komredi Kinana akivishwa kofia ya jadi ya Sungusungu wakati wa mapokezi wilayani…

Siku chache baada ya mwanadada anayefanya vizuri kwenye filamu Bongo, Wema Sepetu ‘Madam’ kutangaza nia ya kugombea ubunge kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), chama hicho kimempa baraka mrembo huyo kwa uamuzi wake huo.

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye alisema kila mwanachama ana haki ya kugombea uongozi wowote ule ilimradi awe mwanachama hai, hivyo kwa Wema kugombea ubunge wa viti maalum ni haki yake na amefanya uamuzi sahihi.

“Kugombea uongozi ni haki ya kila mwanachama, Wema ana haki, kwanza ni mwanachama hai na baba yake alikuwa mwanachama mzuri sana wa CCM mpaka anafariki dunia, hivyo chama chetu huwa hakikutani na watu barabarani tu, bali wanakuwa ni halali kabisa mpaka wanatangaza kugombea,” alisema Nape.

Hata hivyo, alisema wasanii wote waliotangaza kugombea kupitia chama hicho hawajakurupuka bali ni wanachama hai na wamekuwa wakishiriki kwenye shughuli mbalimbali za kichama, tangu kwenye kampeni za mwaka 2010.

Wasanii wengine waliotangaza nia ya kugombea ubunge kupitia CCM licha ya Wema ni Ndumbagwe Misayo "Thea" (Viti Maalum, Kinondoni) na Wastara Juma (Viti Maalum Morogoro Vijijini).